Nyanza-Lac: viongozi wawili wa chama cha CNDD-FDD wafukuzwa nje ya chama

Nyanza-Lac: viongozi wawili wa chama cha CNDD-FDD wafukuzwa nje ya chama

Thaddée Ndayishimiye katibu wa tarafa wa chama tawala na Melack Habonimana aliyeongoza mkutano wa kusimamisha baraza la tarafa ya Nyanza-Lac mkoa wa Makamba (Kusini mwa Burundi) walisimamishwa ndani ya chama tawala. Kulingana na wafuasi wa CNDD-FDD, hatua hiyo ilifahamika jumatatu jioni baada ya mkutano wa viongozi wa eneo hilo wa chama hicho kwa ushawishi wa katibu wa chama ngazi ya mkoa. HABARI ya SOS Médias Burundi

Thaddée Ndayishimiye alituhumiwa kosa la ” kujaribu kusambaratisha uongozi wa chama na kuasi chama kwa kushirikiana na wapinzani wa chama cha CNL “. Anakabiliwa pia kosa la ulevi wa kupindukia.

Melack Habonimana upande wake anatuhumiwa kosa ” la kujiunga na wapinzani hadi kufikia hatua ya kusimamisha baraza la tarafa wakiwa katika eneo lisilojulikana”.

Naibu wa katibu mkuu wa tarafa wa chama cha CNDD-FDD anachikilia kwa muda nafasi ya Thaddée Ndayishimiye.

Vyanzo vyetu vinasema kuwa hakuna aliyeruhusiwa kutoa maoni ndani ya mkutano huo.

” Walialikwa ili kupewa taarifa hiyo” .

Kwa mjibu wa washiriki licha ya kuwa wawakilishi wa chama ngazi za vijiji na vitongoji kuhudhuria, watu wawili peke, Eliezer Ndegeya naibu katibu mkuu wa chama cha CNDD-FDD ngazi ya tarafa na Gilbert Nduwayo katika mkuu wa chama ngazi ya mkoa ndio waliongea.

Washiriki wanazidi kuwa idadi kubwa ya walioalikwa walisusia mkutano huo.

Wanafahamisha kuwa Eliezer Ndegeya alitoa hutba ya uzinduzi akituhumu Thaddée Ndayishimiye makosa yote kabla ya kumpa nafasi ya kuongea Gilbert Nduwayo katibu wa chama cha CNDD-FDD ngazi ya mkoa.

” Mfuasi huyo alifahamisha hatua zilizochukuliwa kabla kwa wafuasi wenzake waliokuwa katika ukumbi wa mikutano wa tarafa, mashahidi wanasema.

Hatua hiyo huenda ilichukuliwa kufuatia rushwa iliyotolewa na Marie Goreth Irankunda mkuu wa tarafa ya Nyanza-Lac aliyesimamishwa hivi karibuni na baraza la tarafa.

Kulingana na wafuasi waliohudhuria mkutano huo ” Tuko na taarifa za uhakika kuhusu utoaji wa rushwa ya pesa inayokadiriwa kuwa milioni moja kwa bwana Nduwayo, katibu wa mkoa wa chama cha CNDD-FDD. Hongo hiyo ilitolewa na Marie Goreth Irankunda ili kumulinda kwenye cheo hicho”. Pesa hiyo ilitoka kwenye kipato cha tarafa ya Nyanza-Lac ambayo ni kati ya maeneo ya nchi yanayoingiza pesa nyingi ikizingatiwa kuwa inapatikana kwenye mwambao wa ziwa Tanganyika.

Gilbert Nduwayo naye anatajwa katika watu waliojipa ardhi za serikali katika kijiji cha Mwimbiro na Bukeye ambazo sasa zinatumiwa na chama cha ushirika cha SANGWE (kinachoundwa kwa sehemu kubwa na wafuasi wa chama cha CNDD-FDD). Tuhuma hizo zinamkabili Marie Goreth Irankunda na ofisi ya baraza la tarafa pia.

Washiriki hao wanakariri uamzi wao wa kuunga mkono hatua ya baraza la tarafa ya Nyanza-Lac ambayo ilichukuliwa ijumaa iliyopita.

Wanaomba rais wa jamuhuri kuunda kamati huru kwa ajili ya kufanya uchunguzi juu ya tuhuma dhidi ofisi ya baraza la tarafa ya Nyanza-Lac kwa ajili ya ” kusimamisha vurugu zinazoshuhudiwa ndani ya tarafa hiyo”.

Ifahamike kuwa wafuasi watatu wa chama tawala waliokuwa wameachiwa huru na polisi hivi karibuni, walisimamishwa tena usiku wa kuamkia jumapili kwa amri ya ofisi ya tarafa.

Muvala, muakilishi wa Imbonerakure ( wajumbe wa tawi la vijana la chama tawala) kwenye kijiji cha Muhuba, Mahuba katibu wa chama cha CNDD-FDD katika kijiji hicho na mkuu wa kijiji hicho anayefahamika kwa jina maarufu Rukanga walikamatwa na polisi walinzi wa mkuu wa tarafa. Mbali na Mahuba aliyefanikiwa kutoroka, wafuasi hao wawili wengine wa chama madarakani wanashikiliwa katika gereza la polisi ngazi ya tarafa.

Marie Goreth Irankunda anayejaribu kujiimarisha katika cheo cha mkuu wa tarafa ya Nyanza-Lac anapata uungwaji mkono kutoka ofisi ya katibu mkuu wa chama tawala. Alifukuzwa kwenye nafasi ya kuongoza mmoja kati ya tarafa za Burundi zinazoingiza pesa nyingi wakati ambapo tarafa hiyo kawaida ilipewa ” mtu wa jinsia ya kiume” jambo ambalo limekuwa likikosolewa bila mafanikio

Previous Kivu-Kaskazini: serikali ya Kongo imepandisha idadi ya waliouwawa eneo la Kishishe
Next Mahama (Rwanda): the education component given to the World Vision