Bijombo: wakaazi wanatuhumu jeshi la Burundi na Kongo kuwapora ng’ombe

Bijombo: wakaazi wanatuhumu jeshi la Burundi na Kongo kuwapora ng’ombe

Vijiji vya Gahuna na Kuwamabuye vinapatikana katika wilaya ya Bijombo. Ni tarafa ya Uvira mkoa wa Kivu ya kusini mashariki mwa DRC. Wakaazi wa vijiji hivyo wanatuhumu wanajeshi wa Burundi na Kongo kuiba ng’ombe 7 na kuchoma moto nyumba eneo hilo. HABARI SOS Médias Burundi

Kwa mjibu wa vyanzo vya ndani, askali jeshi walioiba siku ya jumapili iliyopita, wamepiga kambi eneo la Gahuna.

” Pamoja na ng’ombe kuibiwa, wanajeshi wa FDNB ( jeshi la Burundi) na FARDC ( jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) walichoma moto nyumba”, mashahidi walisema.

Ni wakaazi wa eneo chini ya udhibiti wa wapiganaji wa jamii ya Banyamulenge wanaoongozwa na kanali wa zamani Makanika kwenye kijiji cha Kirumba, kulingana na vyanzo vyetu.

Jeshi la Burundi na Kongo halijasema chochote kuhusu madai hayo. Lakini tarehe 6 disemba 2022, majeshi hayo yalitoa muda wa masaa 24 kwa kanali Makanika kamanda wa kundi la waasi la Twirwaneho kutia silaha kinyume chake, watashambulia ngome zake zote”.

Kulingana na vyanzo vya ndani, majeshi ya Burundi na Kongo tayari yaliweka ngome eneo la Gahuna, Kirumba, Kangwe na pia eneo la karibu na msitu wa Bijabo ambako Makanika aliweka makao yake makuu.

Kwa muda mrefu jeshi la Burundi limekuwa likituhumiwa kuingia nchini DRC likishirikiana na vijana Imbonerakure ( wafuasi wa tawi la vijana wa chama tawala cha CNDD-FDD). Tangu mwishoni mwa agosti mwaka huu, jeshi la FDNB liliingia rasmi nchini humo chini ya jukwa la kikosi cha kikanda lilichoanzishwa na wakuu wa nchi za EAC mwishoni mwa juni mwaka huu kwa lengo la ” kutokomeza makundi ya waasi ya nje na ndani yanavuruga mashariki mwa Kongo ” na ” kurejesha amani na usalama”.
Awamu ya tatu ya mazungumzo ya Nairobi kuhusu mzozo wa mashariki mwa Kongo unaoendelea kwa takriban miongo mitatu hayakuweza kufikia hatua ya ” kusitisha vita”. Mpatanishi katika mgogoro huo, rais wa mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta alifahamisha kuwa ” hatuweza kumaliza mzozo unaomaliza zaidi ya miaka 20 katika siku moja”, akidai kuwa ni njia kuelekea kupata suluhu ya mzozo huo”.

Mahasimu walikubaliana juu ya uundwaji wa kamati ya kujadili njia za kuachilia huru wafungwa wa kisiasa ambao hawakuhusika na mauwaji ya kivita na mauwaji ya kuangamiza jamii.

Previous Bubanza: the provincial court sentenced an Imbonerakure accused of murder to twenty years in prison
Next DRC: serikali inatuhumu Rwanda kutuma kinyume cha wandishi wa habari katika eneo la Rutshuru