DRC: serikali inatuhumu Rwanda kutuma kinyume cha wandishi wa habari katika eneo la Rutshuru

DRC: serikali inatuhumu Rwanda kutuma kinyume cha wandishi wa habari katika eneo la Rutshuru

Serikali ya Kongo kupitia tangazo rasmi, inalaani uwepo kinyume cha sheria wa wandishi wa habari wenye msimamo wa karibu na Rwanda nchini DRC. Msemaji wa serikali ya Kongo amewataja kama watu wanaofanyia propaganda Kigali katika kisa cha mauwaji ya Kishishe. HABARI SOS Médias Burundi

Kupitia tangazo, waziri wa mawasiliano na msemaji wa serikali ya Kongo ametoa tahadhari kuhusu ” kampeni mpya ya uongo wa Rwanda ili kuficha ukweli wa mauwaji ya Kishishe”. Mauwaji hayo yalitokea katika wilaya ya Rutshuru mkoa wa Kivu-kaskazini, mashariki mwa DRC.

” Tunalaani kwa nguvu zote uwepo pasina kuheshimisha sheria wa baadhi ya wandishi wa habari, vyombo vya habari na maafisa wa mawasiliano chini ya ushawishi wa Kigali na kufanya kazi kinyume cha sheria kwenye ardhi ya Kongo”, linasema tangazo lililosomwa na waziri Patrick Muyaya.

Na kuzidi kuwa ” kuanzisha Bunagana hadi Kishishe kupitia Bambo (eneo la Bwito), Murimbi na wilaya ya Tongo na makao makuu ya Rutshuru wandishi wa habari hao wanachungwa na kikosi cha M23/RDF(jeshi la Rwanda)”.

Bwana Muyaya anasema kuwa nia yao ni kutoa taarifa kwa jamii ya kitaifa na kimataifa kuhusu ” uongo wa Rwanda ili kuficha ukweli, kutoa kipau mbele kwa ushahidi wa uongo wa wakaazi na kunyamazisha ukweli wote kuhusu mauwaji ya Kishishe na maeneo mengine”.

Anafahamisha kuwa wizara anayoingoza ina haki ya kutumia njia halali dhidi ya watu wote ” watakaondeleza kampeni hiyo ya uongo ya Kigali kwa kutumia ushahidi wa uongo wa wananchi waliotekwa na kulazimishwa kufanya mchezo huo na wakiwa chini ya vitisho vya kuuwawa”.

” ushirikiano huo wa vyombo vya habari kati ya Rwanda na M23 ni dalili nyingine ya uungwaji mkono wa utawala wa raia Paul Kagame kwa magaidi hao wanaosababisha usalama mdogo katika nchi yetu” alithibitisha.

Alifahamisha kuwa nchi yake iliahidi kuwafungulia mashtaka watuhumiwa wote makosa ya kimataifa wakiwemo mauwaji ya Kishishe na Bambo ili kuhakikisha waathiriwa wanapata fidia.

Kigali bado haijajieleza juu ya madai hayo ya Kinshasa. Lakini hivi karibuni, waziri wa Rwanda na uhusiano wa kimataifa Vincent Biruta alihakikisha kuwa ” M23 halina haki ya kufananishwa na Rwanda. Sio tatizo linalotakiwa kusuluhishwa na Rwanda”, na kutuhumu jamii ya kimataifa ” kuwa mtazamo wao wa kukosea unasababisha tatizo kuwa kubwa”.

kundi hilo la zamani la watutsi lililochukuwa tena silaha mwishoni mwa mwaka 2021 linatuhumu viongozi wa Kongo kutoheshimu ahadi zake kuhusu kuwarudisha katika maisha ya kawaida wapiganaji wake, linaendelea kuomba uchunguzi wa kina juu ya mauwaji ya Kishishe ambapo viongozi wa Kongo wanasema ni raia 272 waliuwawa, Monusco ( kikosi cha umoja wa mataifa nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) kinasema ni idadi ya watu 131 waliuwawa. Waziri wa Kongo wa sheria tayari alipeleka kesi hiyo mbele ya ICC ( mahakama ya kimataifa uhalifu wa kivita), Rwanda ikituhumiwa sambamba na waasi hao na serikali ya Kongo.

Wandishi wa Burundi na Rwanda waliokuwa wakielekea jumatatu hii mjini Bukavu ( makao makuu ya Kivu-kusini ) wamejikuta wakinyimwa ruhsa ya kuvuka mpaka. Wangehudhuria katika mafunzo yaliandaliwa na la Benevolencia shirika la kihisani ya uholanzi linalounga mkono vyombo vya habari vingi katika ukanda wa maziwa makuu ya afrika. Wenzutu hao wamelazimika kufanya mafunzo hao eneo la Kamembe ( Rwanda) ambapo wajumbe kutoka Kongo waliwasili kulingana na wahusika. Haijabainika wazi kuwa ni kutokana na tangazo la msemaji wa serikali Patrick Muyaya ambapo wahudumu katika idara ya mawaliano wametuzuia kuingia kwenye ardhi ya Kongo. ” wamewafahamisha tu kuwa la ” Benevolencia haikuomba ruhsa kwenye wizara ya vyombo vya habari.

Previous Bijombo: wakaazi wanatuhumu jeshi la Burundi na Kongo kuwapora ng'ombe
Next North Kivu: meeting between the M23 and the FARDC