Burundi: ni nani waliomuteka mwandishi wa habari Jérémie Misago ?

Burundi: ni nani waliomuteka mwandishi wa habari Jérémie Misago ?

Mwenzetu hajulikani alipo tangu jumamosi iliyopita. Jumatatu hii, ameonekana ndani ya video akidai kuwa yuko salama bila hata hivyo kufahamisha malaha alipo. HABARI SOS Médias Burundi

Ni majira ya mchana ambapo video hiyo imetumwa kwa watu wake wa karibu. Mwandishi huyo ameonekana kama mtu aliyetulia. Amesema kuwa ” yuko salama” lakini hakubiani mahala alipo. Anafahamisha tu kuwa ” atasema yaliomukuta”.

Katika video hiyo isiokuwa ya kawaida”, mwandishi huyo Jérémie Misago anaeleza : ” Nilijikuta katika eneo hili la nchini kati bila kujuwa . Sikupanga hayo, ningepanga ningewafahamisha watu wa karibu na marafiki. Amehakikisha kuwa angewasili Bujumbura jumatatu jioni au jumanne asubuhi.
Mwenzetu huyo alionekana akiwa na mudhaifu, chini ya vitisho, akiwa amechoka na kuonekana kuogopa mtu aliyekuwa pembeni yake, akilazimika kukariri kwa vitu.
Katika tangazo, gazeti la Iwacu halikupenda kutoa maelezo zaidi na kupongeza polisi kwa “ushirikiano wake mzuri”.

Msemaji wa polisi ya Burundi (PNB), Désiré Nduwimana ametuhakikishia kuwa “polisi inafahamu tatizo hilo, vyombo vya usalama vinafanya kazi yao. Tutawambia maendeleo”.

Kwa mjibu wa mtalaam katia sayansi ya mawasiliano, kuona mwenzetu ameamuru kutuma video kuliko kurudi nyumbani ni jambo linaloleta wasi wasi.

“Ni ajabu. Katika hali kama hiyo, jambo la kwanza, mwandishi Jérémie Misago angetakiwa kurudi nyumbani kuliko kuchukua vidéo” amebaini mtalaam huyo.

Previous Bukinanyana: waasi wa Rwanda wameuwawa na wengine kukamatwa
Next Cibitoke: three judicial police officers and an administrative officer detained for murder and corruption