Bukinanyana: waasi wa Rwanda wameuwawa na wengine kukamatwa

Bukinanyana: waasi wa Rwanda wameuwawa na wengine kukamatwa

Siku chache zilizopita, mapigano kati ya jeshi la Burundi dhidi ya watu wenye kubebelea silaha yalifanyika. Makabiliano yalifanyika katika msitu wa Kibira kwenye tarafa za Mabayi na Bukinanyana (mkoa wa Cibitoke, kaskazini magharibi mwa Burundi). HABARI SOS Médias Burundi

Vyanzo vya ndani vinafahamisha kuwa angalau waasi saba waliuwawa na wengine wanne kukamatwa.

Kwa mjibu wa mashahidi, mapigano makali yalisababisha wasiwasi miongoni mwa wananchi.

” Mapigano yalikuwa makali. Wanajeshi wa Burundi waliwashitukia waasi wa Rwanda na kuwashambulia ambao upande wao walijihami. Tayari miili saba imepatikana na waasi wane kukamatwa “. wanathibitisha mashahidi.

Kukimbia

Vyanzo katika jeshi ambao majina yalihifadhiwa wanaeleza kuwa walipewa amri ya kuwafurusha waasi. Na kuzidi kuwa : ” hata hivyo taarifa zilivuja .Tuko na uhakika kuwa walifahamu kuhusu mpango wetu wa kuwashambulia. Ni jambo lisilorahishishia idara ya upelelezi ili kutoa muelekeo wa operesheni uwanjani ” wanalaani.

Hofu

Familia nyingi zililazimika kutoroka makaazi yao wakihofia usalama wao,…..tuliyajuwa hayo. Mkuu wa tarafa ya Bukinanyana aliwaomba wakaazi kuwafichua wanaoshirikiana na waasi.
Kiongozi mmoja wa kijeshi alisisitiza juu ya kile alisema ” hali imedhibitiwa ” bila kutoa maoni yoyote kuhusu mapigano hayo yaliyoripotiwa na vyanzo vya ndani.

Previous Ituri: a new attack by ADF rebels leaves dead and injured in Irumu
Next Burundi: ni nani waliomuteka mwandishi wa habari Jérémie Misago ?