Rwanda-DRC : jeshi la Rwanda lashambulia ndege ya kivita ya Kongo ndani ya anga ya Kongo (Tangazo)

Rwanda-DRC : jeshi la Rwanda lashambulia ndege ya kivita ya Kongo ndani ya anga ya Kongo (Tangazo)

Serikali ya Kongo inatuhumu jeshi la Rwanda kushambulia ndege yake ya kivita ya Kongo ndani ya anga ya DRC. Ni kulingana na tangazo la viongozi wa Kongo la jumanne hii jioni, wakijibu tuhuma za serikali ya Rwanda kuwa jeshi la Kongo lilivamia anga ya Rwanda alasiri. Nchi hizo mbili zinatuhumumiana kuchokozana”. HABARI SOS Médias Burundi

Katika tangazo la serikali ya Kongo la usiku, viongozi wa nchi hiyo kubwa ya afrika ya kati wanafahamisha kuwa ” serikali ya Kongo inalaani vikali shambulizi dhidi ya ndege yake ya kivita lililofanywa na jeshi la Rwanda katika anga ya Kongo na haitakubali hali hiyo”.

” Ndege hiyo ya kivita ilishambuliwa wakati ikituwa kwenye uwanja wa kimataifa wa Goma ( makao makuu ya Kivu-kaskazini)”, linatuhumu tangazo la serikali ya Kongo ambalo linazidi kuwa” kombora la Rwanda lilielekezwa kwenye ndege ya Kongo iliyokuwa ndani ya ardhi ya Kongo”.

Ndege ya kivita haikuvamia anga ya Rwanda, walifahamisha viongozi wa Kongo wanaojipongeza kuwa iliweza kutuwa bila madhara makubwa.

Madai mapya

Serikali ya Kongo inatuhumu pia jeshi la Rwanda kuwatuma wanajeshi wake jumanne hii eneo la Kitchanga kwenye umbali wa kilometa 80 kaskazini magharibi mwa Goma.

” Shambulio hilo lilifuata mapigano ya jumanne hii ya jeshi la Rwanda eneo la Kitchanga na kurudishwa nyuma na jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo (FARDC). Wakati huo huo ulishuhudiwa msafara wa wanajeshi wa Rwanda kwa ajili ya kuimarisha ngome maeneo ya Kibumba na Bwito kuandaa mashambulizi mengine”, serikali ya Kongo inalaani.

Viongozi wa Kongo wanasema ” ni kisa cha uchokozi sawa na kuanzisha vita”. Lengo la Rwanda ni kuvuruga juhudi katika kutekeleza makubaliano ya mchakato wa Luanda( Angola) na Nairobi (Kenya) kwa ajili ya kurejesha amani mashariki mwa DRC na kanda ya maziwa makuu.

Kuvuruga uchaguzi

Serikali ya Kongo inafahamisha kuwa zoezi la kuorodhesha wapiga kura mashariki mwa Kongo na kati kati litaanza katika siku zijazo. Inaomba jamii ya kimataifa kuendelea na shinikizo dhidi ya serikali ya Rwanda na kundi la M23 ili waweze kusimamisha vurugu ambazo zinaweza kuharibu mchakato wa uchaguzi kwa mjibu wa viongozi wa Kongo.

Hivi karibuni, rais wa Rwanda alijieleza kuhusu ndege ya kivita ya Kongo kuvamia anga ya nchi yake. Rais Paul Kagame alitaja vitendo hivyo vilivyofanyika mara tatu tangu novemba 2022 kama ” mialiko”.

” Nafikiri kuwa nilipata mialiko ya kutosha ili niweze kujibu. Kwanza bomu lilivurumishwa kutoka upande wa pili, harafu wanajeshi wenye silaha walivuka mpaka na kujaribu kupiga risasi maafisa wanaolinda usalama wa mipaka au ndege ndege kuingia katika ardhi yetu. Tulijizuia kujibu mwaliko huo. Lakini sijuwi kama subra hiyo itaendelea kwa kwa muda gani iwapo watarudi tena”, alitahadharisha mwezi disemba rais Paul Kagame mbele ya bunge la Rwanda.

Uhusiano kati ya mataifa hayo ya maziwa makuu ya afrika unazidi kuzorota tangu kuibuka upya kundi la machi 23, M23.

Kundi hilo la waasi wa watutsi lilichukuwa tena silaha mwishoni mwa 2021 likituhumu viongozi wa Kongo kutoheshimu ahadi zake kuhusu kuwarejesha katika maisha ya kawaida wapiganaji wake ambao ni kutoka Kabila la watutsi wa Kongo.

Viongozi wa Kongo wanakubaliana kuwa kundi hilo linapata usaidizi kutoka Rwanda, madai ambayo serikali ya Rwanda inaendelea kukanusha.

Baada ya kudhibiti maeneo mengi ya mkoa wa Kivu-kaskazini mashariki mwa DRC likiwemo eneo la Bunagana jiji la mpakani na Uganda na kutishia kuchukuwa mji wa Goma makao makuu wa Kivu kaskazini tangu juni iliyopita, waasi wa kundi la M23 waliachia ngome zake za Kibumba ( wilaya ya Nyiragongo) kwa kikosi cha kanda ya EAC wiki chache zilizopita. Hata hivyo, mkuu wa majeshi ya Kongo akituhumu waasi kukataa kuondoka katika maeneo chini ya udhibiti wao. Félix Tshisekedi alitoa tuhuma hizo katika mkutano wa kiuchumi wa Davos.

Serikali ya Kongo inatuhumu pia kundi la M23 kufanya mauwaji ya watu 272 katika vijiji viwili chini ya udhibiti wao, UN ikisema ni watu 130 waliuwawa.

Kundi la M23 linakanusha tuhuma hizo na kuzitaja kama ” propaganda” kwa lengo la kuharibu sura ya kundi hilo mbele ya wananchi ” na kuomba uchunguzi huru ufanyike.

Rwanda upande wake inatuhumu jeshi la FARDC ( jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) kushirikiana na kundi la FDLR kwa lengo la kuvuruga ardhi ya Rwanda.

Lakini rais wa Kongo Félix Tshisekedi kwa mara nyingi ilituhumu mwenzake wa Rwanda Paul Kagame kuunga mkono waasi na kudai kuwa “FDLR sio tena tishio kwa Rwanda na kulitaja kundi hilo kama kundi lililogeuka la wezi”.

Kwa mara nyingi kuanzia disemba hadi januari, rais Paul Kagame alituhumu jamii ya kimataifa ” kupendelea viongozi wa Kongo kwa ajili ya kulinda maslahi yake na kusifia amani ya mdomoni”.

Previous Mahama (Rwanda) : zaidi ya wakimbizi elfu moja hawajapewa mlo wao tangu miezi mitatu iliyopita
Next Burundi : kitita cha milioni 21 chatolewa na benki ya afrika ya maendeleo kwa ajili ya kuendeleza sekta ya kilimo