Mahama (Rwanda) : zaidi ya wakimbizi elfu moja hawajapewa mlo wao tangu miezi mitatu iliyopita
Zaidi ya wakimbizi elfu moja idadi kubwa wakiwa kutoka Burundi hawapewa chakula sasa ni miezi mitatu. Kawaida, wanapewa chakula kila baada ya mwezi. Wakimbizi wanapewa pesa za Rwanda kwenye kadi zao. Wahusika hao wanaomba wizara ya Rwanda ya wakimbizi kutafuta suluhu la tatizo hilo. HABARI SOS Médias Burundi
Ni nyakati za kupata msaada wa chakula kupitia pesa ndani ya kambi ya Mahama nchini Rwanda kwa ajili ya mwezi huu wa januari 2023. Hata hivyo zaidi ya wakimbizi elfu moja wanasuburi kupewa bila mafanikio tangu miezi mitatu iliyopita.
” Jifikirie hatuna chakula mimi na familia yangu ya watu watano tangu mwishoni mwa novemba. Ninawadai chakula changu cha miezi mitatu. Kuna wananchi wenzangu wanaodai malimbikizo ya miezi miwili. Baya zaidi PAM (WFP) haitusikilizi”, analalamika baba mmoja wa familia. Yeye na wakuu wengine wa familia wako kwenye mstari mbele ya muhudumu wa benki eneo la Mahama kushuhudia kwa masikitiko makubwa kuwa kadi zao hazina pesa.
Idadi kubwa ya wale ambao majina hayakuonekana kwenye orodha ya wanaopewa msaada ni wale wa levo ya kijamii ya kwanza na ya pili. Mkimbizi wa levo ya kwanza hupewa franka za Rwanda 7.000 ( takriban 7 USD) yule wa pili hupewa nusu ya kitita hicho.
Wakimbizi wamewekwa katika viwango kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa na HCR pamoja na serikali iliowapokea.
” Tumechoka sababu tumetelekezwa. Tunaeleza matatizo yetu kwa HCR ambayo upande wake inatutuma katika shirika la PAM ambayo upande wake inatuelekeza kwenye benki ya Equity inayorasibu pesa yetu ndani ya kambi. Benki hiyo upande wake inatueleza kuwa haijapata orodha yetu kutoka PAM, tunajielekeza kwa wahudumu wa Equity Bank eneo la Kabeza. Wanaotuambia kauli kama hiyo : Hawatuoni kwenye mfumo wao”, walalamika wakimbizi waliojieleza kwa SOS Médias Burundi.
Disemba 2022, CBDH/VICAR, shirika linalotetea haki za wakimbizi lilitoa tahadhari na kujaribu kuuliza zaidi kwenye benki ya Equity.
” Benki ilijibu kuwa inajaribu kufanya matengenezo ili kuwahudumia wakimbizi hao”, alifamisha Léopold Sharangabo naibu kiongozi wa shirika hilo.
Baada ya mwezi mmoja, tatizo halijasuluhishwa. Baya zaidi, orodha ya watu wanaolalamika inazidi kuongezeka kila mwezi.
” Hali hiyo inaonyesha kuwa tulitelekezwa. Ikiwa ni HCR, PAM au benki ya Equity iliyopata soko la kuwapa pesa taslimu wakimbizi, wote hao ni washirika na wanahusishwa katika umasikini wetu, wanashambulia wakimbizi wa Mahama.
Wanaomba wizara ya Rwanda inayohusika na wakimbizi kumaliza hali hiyo inayohatarisha mazingira ya maisha yao ambapo wanasema hali hiyo inaweza kuwapelekea wakimbizi kuchukuwa hatua mbaya ya kurejea makwao kwa nguvu”.
Kambi ya Mahama inapatikana katika mashariki mwa Rwanda. Ina wakimbizi zaidi ya elfu 45 idadi kubwa wakiwa warundi wanaosalia wakiwa raia wa Kongo.
About author
You might also like
Nduta (Tanzania) : an SOS for a dying child
The camp administration has denied access to care for a child under five who requires intensive care outside Nduta camp in Tanzania. The NGO MSF (Médecins Sans Frontières) finds itself
Nduta (Tanzania): a young Burundian refugee who disappeared, was found dead
Mélance Kwizera, in his twenties, had disappeared last week then found dead near the camp and was quickly buried by the local community who demand investigation. INFO SOS Médias Burundi
Bubanza: two former refugees from Rwanda arrested
President Ndayishimiye’s speech begins to claim victims. Two men from the commune of Musigati and Bubanza, in the province of Bubanza (western Burundi) were arrested by the police on Monday.