Burundi : kitita cha milioni 21 chatolewa na benki ya afrika ya maendeleo kwa ajili ya kuendeleza sekta ya kilimo

Burundi : kitita cha milioni 21 chatolewa na benki ya afrika ya maendeleo kwa ajili ya kuendeleza sekta ya kilimo

Mikoa ya kaskazini mashariki mwa Burundi ambayo ni : Ngozi, Kirundo na Muyinga itanufaika na mradi hui kwa kutengeneza mabonde ya mito mingi. Lengo ni kuongeza mavuno ya kilimo kwa ajili ya kukabiliana na usalama mdogo wa chakula. HABARI SOS Médias Burundi

Mradi huo ulizinduliwa alhamisi iliyopita katika mkoa wa Kirundo kaskazini mwa nchi. unahusika na kuongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo na ufugaji.

Dola za kimarekani milioni 21 zilitolewa kwa serikali ya Burundi na banki ya afrika kwa ajili ya maendeleo (BAD).

Mjumbe wa BAD katika nchi hiyo ndogo ya afrika mashariki alifahamisha kuwa “Tunashirikiana na serikali katika mipango yake”.

Mradi huo wa kuunga mkono maendeleo endelevu ya kilimo na ufugaji nchini Burundi ( PADCAE_B) utatekelezwa katika mikoa ya Ngozi, Kirundo na Muyinga.

Utasaidia katika kukabiliana ya uhaba wa chakula na kuendeleza ajira kwa vijana na kutekeleza kilimo cha uhakika.

Madhumuni kulingana na mjumbe wa BAD ” kuhakikisha kuwa watu milioni tatu katika maeneo hayo matatu yaliyochaguliwa wamepata uwezo wa kuzalisha vya kutosha”.

Waziri wa kilimo Sanctus Niragira alifahamisha kuwa mradi huo ulianzishwa kwa lengo la kupata suluhu la tatizo la usalama mdogo wa chakula nchini Burundi “.

Mradi huo wa miaka minne utatamatishwa mwishoni mwa juni 2026.

Shughuli zinazopangwa kufanyika ni pamoja na kutengeneza katika mfumo wa kisasa bonde la mto Nyamuswaga linalogusa mikoa ya Muyinga na Ngozi, bonde la Nyamabuno linalogusa mikoa ya Muyinga na Kirundo. Mito ya Rucikiri mkoani Muyinga, Ruyongwe katika mikoa ya Kirundo -Ngozi na Muyinga pamoja pia na Ruganirwa unaopatikana katika mkoa wa Kirundo utahusika pia.

Waziri Niragira aliwaomba raia wanaolengwa na mradi huo ” kujari uwezo wanaopewa kwa ajili ya kuendeleza mradi huo”.

Previous Rwanda-DRC : jeshi la Rwanda lashambulia ndege ya kivita ya Kongo ndani ya anga ya Kongo (Tangazo)
Next Makamba : chumba cha kuhifadhi maiti hakifanyi kazi kwa takriban mwaka mmoja sasa