Makamba : chumba cha kuhifadhi maiti hakifanyi kazi kwa takriban mwaka mmoja sasa

Makamba : chumba cha kuhifadhi maiti hakifanyi kazi kwa takriban mwaka mmoja sasa

Kwa mjibu wa wafanyakazi kwenye hospitali hiyo ya Makamba ( kusini mwa Burundi) pamoja na familia zilizokosa watu, chumba cha kuhifadhi maiti sasa ni takriban mwaka mmoja kikiwa hakifanyi kazi. Baadhi ya familia wanalalamika kuwa miili ya watu wao inaharibika kabla ya kuzikwa. Hata hivyo bili ya kuhifadhi maiti ndani ya chumba hicho inazidi kutolewa, ni franka elfu 15 kwa kila siku wakati ambapo chumba hicho hakifanyi kazi. Wakaazi wanaomba kitengenezwe mara moja. HABARI SOS Médias Burundi

Familia moja inafahamisha kuwa ilipata matatizo katika mazishi ya mmoja kati ya wajumbe wake aliyefariki baada ya siku nne muili wake ukiwa ndani ya chumba cha hospitali hiyo cha kuhifadhi maiti.

Wanaeleza kuwa ” hatukuweza kuweka muili ndani ya sanduku sababu maiti ilikuwa imeharibika sana”.

Familia nyingi zinalalamika kupeleka miili ya wajumbe wao waliofariki katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali za Bururi na Rutana ( Kusini mashariki mwa Burundi).

” Mchakato huo unatugharimu pesa nyinshi kwa kukodi gari la kubeba maiti safari ya kwenda na kurudi na kujumulisha pia gharama za chumba hicho”, wanalaani familia hizo.

Taarifa hizo zinahakikishwa na wafanyakazi kwenye kituo hicho cha afya.

Viongozi wa hospitali hiyo hadi sasa bado hawajapata suluhu la tatizo hilo.

Wafanyakazi kwenye hospitali hiyo wanadai kuwa ” ni aibu kwa hospitali kuu ya mkoa inayowapokea wagonjwa kutoka mkoa wote”.

Wanajiuliza sababu zinazopelekea viongozi wa hospitali hiyo kuacha kutengenezesha chumba hicho wakati ambapo hospitali hiyo ni moja kati ya zile zinazoomba gharama kubwa ya kuweka maiti ndani ya chumba cha kuhifadhi maiti.

Familia za wahanga na wafanyakazi wa hospitali ya Makamba wanaomba viongozi wakuu katika sekta ya afya kushinikiza ili viongozi wa kituo hicho cha afya watengenezeshe chumba hicho.

Wiki iliyopita, walikuwa walionekana kuanza kutengenezesha chumba hicho cha kuhifadhi maiti wakati wa ziara ya waziri wa afya katika mkoa huo lakini kazi zilisimama kwa mjibu wa mashahidi.

Previous Burundi : kitita cha milioni 21 chatolewa na benki ya afrika ya maendeleo kwa ajili ya kuendeleza sekta ya kilimo
Next Kirundo : two men sentenced to life jail for the murder of a woman