Masisi : hofu imetanda eneo la Sake kutokana na mapigano kati ya jeshi na kundi la M23

Masisi : hofu imetanda eneo la Sake kutokana na mapigano kati ya jeshi na kundi la M23

Hali ya taharuki imeshuhudiwa alhamisi hii ndani ya jiji la Sake kwenye umbali wa takriban kilometa 20 magharibi ya mji wa Goma( makao makuu ya mkoa wa Kivu kaskazini) mashariki mwa Kongo kutokana na mapigano kati ya jeshi la Kongo na waasi wa M23. Familia nyingi zimetoroka makaazi yao na kuelekea katika mji mkuu wa mashariki mwa DRC. HABARI SOS Médias Burundi

Ma mia ya wakaazi wamekimbia na kuelekea Goma ndani ya kambi za wakimbizi na familia za mapokezi alhamisi hii tarehe 9 februari 2023. Kwenye barabara ya Goma_Sake, ma lori na pikipiki vinavyosafirisha wakimbizi wa ndani na wengine katika makundi wakitembea na miguu pamoja na watoto wao mikononi wakikimbia mingurumo ya silaha kubwa na ndogo ndogo inayosikika katika eneo hilo.

Tunatoroka sake sababu hali imekuwa mbaya eneo hilo. Waasi wako karibu na jiji la Luhonga ambako wamezungukia “, anaeleza Murisho , mkaazi aliyetoroka eneo hilo.

Mashirika ya kiraia ya kitongoji cha Kamuronza ( eneo hilo hilo wanaonekana kutokubaliana na hali kama inavyoelezwa na kuthibitishwa kuwa hali inadhibitiwa na mapigano yanaendelea mbali ya jiji hilo.

” Ni waasi wa Mai Mai waliokuwa na lengo la kuingia hapa lakini kila kitu kinaendelea vizuri. Mapigano yanaripotiwa kwenye umbali wa kilometa takriban 10 ya Sake kuelekea Lupango” alifafanua kiongozi wa polisi eneo la Sake ambaye anawatolea mwito wananchi kuwa watulivu.

Mapigano makali yaliriripotiwa tangu wiki moja iliyopita kati ya jeshi la Kongo na waasi wa M23 ndani ya vitongoji vya Kamuronza na Matanda katika wilaya ya Masisi. Jeshi linajaribu kuhimili kundi hilo la silaha kwa kutumia makombora makubwa pamoja na mashambulizi ya angani.

Kundi hilo la zamani la watutsi, lilichukuliwa tena silaha mwishoni mwa 2023 na kuwatuhumu viongozi wa Kongo kuacha kutekeleza ahadi zake za kuwarejesha katika maisha ya kawaida wapiganaji wake. Kundi hilo linadhibiti maeneo mengi ndani ya mkoa wa Kivu-kaskazini tangu juni 2021, likiwemo la Bunagana, jiji la mpakani na Uganda .

Viongozi wa Kongo wanakubaliana kuwa kundi hilo linapata usaidizi kutoka Rwanda huku serikali ya Rwanda upande wake ikitupilia mbali madai hayo na kutuhumu Kinshasa kushirikiana na kundi la waliotekeleza mauwaji ya halaiki la FDLR kwa kuwapa silaha, sare za jeshi na risasi kwa lengo la kuvugana ardhi yake.”

Previous Nyarugusu (Tanzania) : mashamba mengi ya mahindi kuharibiwa na uongozi wa kambi hiyo
Next Zambia : karibu warundi 30 wanazuiliwa jela kwa kosa la uhamiaji haramu