Nyarugusu (Tanzania) : mashamba mengi ya mahindi kuharibiwa na uongozi wa kambi hiyo

Nyarugusu (Tanzania) : mashamba mengi ya mahindi kuharibiwa na uongozi wa kambi hiyo

Visa hivyo vimeripotiwa mwanzoni mwa wiki hii katika kambi ya Nyarugusu nchini Tanzania. Mkuu wa kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu aliharibu shamba la mahindi kwa ajili ya kupiga vita shughuli zote za kilimo. HABARI SOS Médias Burundi

Jumatatu na jumaa nne hii, uongozi katika kambi ya Nyarugusu pamoja wa walinzi walijihusisha na kuzunguuka kambi kwa ajili ya kuangalia mashamba yote ya mahindi katika eneo la kambi linalokaliwa na warundi.

“Walizunguuka katika vijiji huku wakiimba nyimbo kama watu wanaofanya kazi nzuri. Maeneo matano (7, 8, 9, 10 na 11) ndio yalichaguliwa. Mashamba yote yaliharibiwa. Ni maskitiko makubwa kuona binadamu akiharibu shamba mchana kweupe. Ni uhalifu mtupu”, anakosoa mkimbizi kutoka Burundi.

Kuna upendeleo

” inasikitisha kuona sehemu inayokaliwa na raia wenye asili ya Kongo haikulengwa. Je, sisi wote si wakimbizi ambao haki zetu zinalingana ? “, anajiuliza mkimbizi mmoja ambaye aliambia SOSMedias Burundi.

Uongozi wa kambi ulifahamisha kuwa ni kwa ajili ya kuwazuia kufanya kilimo wakimbizi ambao wanalazimika kujiorodhesha ili waweze kurudi makwao kwa hiari”.

Hata hivyo, warundi kupitia kitendo hicho wanaona kuwa ni ” njia ya kuwalazimisha kurudi nyumbani kwa nguvu. Hayo yanafanyika wakati HCR yenye jukumu la kuwalinda ilishuhudia”.

Kilimo kilikuwa na mazao mazuri msimu hii, mwaka mmoja baada ya kuvuna mboga boga na maharagwe. Kwa sasa , wakimbizi walitumia fursa hiyo ili kupanda mbegu za mahindi.

” Ndani ya shamba la maharagwe, miti 5O angalau ilipandwa sehemu hiyo. Lakini watu hao hawakuacha kukata na migomba ya mahindi ” , alaani mkimbizi mmoja.

Nyarugusu ni kambi ambayo haikuitikia mpango wa kurejesha wakimbizi kwa hiari wakati ambapo HCR na serikali ya Burundi walikubaliana kurejesha wakimbizi zaidi ya elfu 70 mwaka huu wa 2023 hususan wale kutoka Tanzania ambayo iliwapa hifadhi kwa wakimbizi wa Burundi zaidi ya 145 elfu katika kambi mbili ya Nduta na Nyarugusu kulingana na HCR.

Previous Ngozi: uhaba wa chakula kwenye gereza kuu
Next Masisi : hofu imetanda eneo la Sake kutokana na mapigano kati ya jeshi na kundi la M23