Ngozi: uhaba wa chakula kwenye gereza kuu

Ngozi: uhaba wa chakula kwenye gereza kuu

wafungwa katika gereza kuu la Ngozi (kaskazini mwa Burundi) wanasema kuwa wanateseka kutokana na ukosefu wa chakula. Walioathirika zaidi ni wale wanaotoka katika mikoa ya Kirundo na Kayanza (kanda hiyo hiyo). Wanadai kuwa hawapati wageni kama wenzao wenye asili ya mkoa wa Ngozi kutokana na masafa marefu ambayo wajumbe wa familia zao wanatakiwa kufanya ili kufika kwenye gereza hilo. Wagonjwa hawawezi kumeza dawa wakati ambapo hakuna kitu tumboni. Wanaomba misaada. HABARI SOS Médias Burundi

Gereza hilo linawahifadhi wafungwa kutoka mikoa ya Ngozi, Kayanza, na Kirundo. Wafungwa katika gereza hilo wanaishi katika mazingira magumu kutoka na uhaba wa chakula.

” Wiki mbili zimemalizika pasina kupewa maharagwe. Ili kuweza kula ugali wao mdogo, baadhi hununua mboga boga lakini kwa wale ambao hawana uwezo, hutumia maji ya moto yaliyowekewa chumvi. Inakasirikisha “, anahakikisha mfungwa mmoja mwenye asili ya mkoa wa Kayanza.

“Tumezoea kula mara moja kwa siku nyakati za mchana peke”, alifamisha mfungwa mmoja.

Habari kutoka katika gereza hilo zinafamisha kuwa wafungwa wenye asili ya mikoa ya Kirundo na Kayanza wanaathiriwa zaidi na hali hiyo sababu wanakuwa mbali na familia zao zinazolazimika kusafiri masafa marefu ili kuweza kuwatembelea.

” Angalau hao wenye asili ya mkoa wa Ngozi wanapata urahisi kidogo kwa sababu wajumbe wa familia zao wanaweza kuwatembelea angalau mara tatu kwa wiki. Lakini sisi njaa inatumenya. Tunaweza kupata mgeni mara moja kwa mwezi”,alilalamika mfungwa mwengine.

Maradhi ya utapia mlo yanaanza kusambaa.

Wafungwa wenye maradhi yasiopona ambao wanalazimika kula kabla ya kutumia dawa wanaathiriwa zaidi na hali hiyo.

” wafungwa wenye HIV wanalazimika kutumia dawa pasina kula. Baadhi wanaanza kupata maradhi ambayo walikuwa hawana kama kuumwa tumbo, alitoa ushuhuda huo mfungwa wa zamani.

Gereza la Ngozi linawapa hifadhi wafungwa zaidi ya 1500 wakati uwezo wake ni kuwapokea watu 400 peke.

Previous Masisi : strong tension in Sake following the fighting between the army and the M23
Next Nyarugusu (Tanzania) : mashamba mengi ya mahindi kuharibiwa na uongozi wa kambi hiyo