Kivu-kaskazini: Jeshi na kundi la M23 wanapigana eneo la Rutshuru karibu na RN2

Kivu-kaskazini: Jeshi na kundi la M23 wanapigana eneo la Rutshuru karibu na RN2

Mapigano kati ya jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo na kundi la machi 23 yameshika kasi alhamisi hii 27 oktoba 2022 katika maeneo ya Chimirwa kwa takriban kilometa 4 kutoka barabara nambari mbili (RN2). Si mbali sana na kijiji cha Ntamugenga katika wilaya ya Rutshuru mkoa wa Kivu ya kaskazini mashariki mwa DRC. Barabara RN2 ni barabara kuu inayotumiwa kuwahudumia wanajeshi hasa katika ukanda huo. Mapigano mengine yameripotiwa upande wa kijiji cha Kibunge kwenye mlima ulio juu ya Kalengera. Vyanzo maeneo hayo vinaarifu kuwa waasi wa M23 wamejaribu kusonga mbele na kupanua maeneo yao lakini wamekujigonga kwenye ulinzi wa FARDC. Mapigano hayo yamepelekea wananchi wengi kukimbia. HABARI SOS Medias Burundi

Milio ya silaha nzito na za kawaida imesikika katika ukanda huo hadi wakati huu.

Makabiliano yameripotiwa katika maeneo mengi ya vijiji vya wilaya ya Rutshuru kivu kaskazini.

” Nilikuwa Kako ambako kuna idadi kubwa ya wanajeshi wa FARDC na pia Rubare. Waasi wameshambulia kuelekea Kibunge juu ya Kalengera. Wako kwenye mstari kuelekea kwenye maeneo ambako Berky inajenga. Wakaazi wa Kako wametoroka makaazi yao, ameelezea mkaazi mmoja.

Wakaazi kutoroka kwa wingi.

Idadi kubwa ya wakaazi wa vituo vya Kako na Rubare wanaelekea kwenye makau makuu ya Rutshuru na Kiwanja.

“Watoto na akinamama wajawazito pamoja pia na watu wazima wanajilazimisha kutembea masafa marefu kwa ajili ya usalama wao na magari mengi zikiwemo za uchukuzi wa watu yaliyokuwa yakitoka Goma ( makao makuu ya Kivu kaskazini) na kuelekea katika mji wa Butembo yamelazimika kurudi ndani ya mji wa Goma”, amebaini mkaazi wa Kako.

Chanzo kingine kimefahamisha kuwa mapigano yamesogea karibu ya kijiji cha Rubare. Wote waliosalia katika mji huo wanajificha ndani ya majumba. Hakuna kutoka nje.

Mapigano kati ya jeshi la FARDC na kundi la M23 yaliibuka tena tangu alhamisi 20 oktoba 2022 katika ukanda wa Rangira-Rwanguba wilayani Rutshuru, baada ya wiki kadhaa za utulivu kabla ya mapigano hayo kutanda kwenye milima mingine.
Mashirika ya kiraia yanatuhumu waasi wa M23 kupiga mabomu kwenye ngome kadhaa za jeshi, ambapo mabomu hayo yalisababisha vifo vya raia 5 na kujeruhi wengine zaidi kulingana na jeshi la Kongo.

Lakini kundi la M23 linatupilia mbali madai hayo. Linafahamisha kuwa badaya yake lilijihami baada ya ngome zake kushambuliwa na jeshi la FARDC kwa ushirikiano na makundi ya silaha yakiwemo kundi la FDLR na Mai Mai.

Previous Rwanda-DRC: DRC imetuhumu kwa mara nyingine Rwanda kusaidia kundi la M23 (tangazo)
Next Bubanza: vijana Imbonerakure 3 wamepinga kuripoti mbele ya askali polisi wa kupeleleza makosa