Rwanda-DRC: DRC imetuhumu kwa mara nyingine Rwanda kusaidia kundi la M23 (tangazo)
Serikali ya Kongo imetuhumu kwa mara nyingine Rwanda kuunga mkono kundi la machi 23, kundi hilo la waasi linalopigana dhidi ya serikali ya jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, tunasoma hayo katika tangazo la serikali ya Kongo la tarehe 25 oktoba 2022. Viongozi wa Kongo wanamuhusisha pia rais wa Rwanda Paul Kagame. HABARI SOS Médias Burundi
Serikali ya Kongo ilikuwa ikizungumzia tangazo la serikali ya Rwanda la siku moja iliyopita ambalo linatupilia mbali tuhuma za kusaidia kundi la M23.
” Yaliyomo ndani ya tangazo kwa wandishi wa habari yanaonyesha wazi kuwa Rwanda inakubali kuwa inaunga mkono waasi wa M23″ hayo yanasomeka katika tamko lililosainiwa na Patrick Muyaya Katembwe, waziri wa mawasiliano na vyombo vya habari na pia msemaji wa serikali ya Kongo.
DRC inamtuhumu binafsi rais wa Rwanda Paul Kagame na kusema kuwa ana mwenendo unaoonyesha vizuri mkakati wake wa kujiingiza daima katika maswala ya ndani ya DRC” ili kudumisha hali ya usalama mdogo mashariki mwa nchi hiyo kubwa ya afrika ya kati.
Rwanda imetuhumiwa kuvunja ahadi ilizochukuwa mjini Nairobi (Kenya), Luanda (Angola) na New York katika michakato mbali mbali ya kutafuta amani na kutokomeza makundi ya waasi kwenye ardhi ya Kongo likiwemo kundi la M23.
Serikali ya Kongo inatupilia mbali kile inachosema ” Maneno yasiyo ya uadilifu ” ya Rwanda na shughuli zake za kijeshi kwenye ardhi ya Kongo na kukumbusha kuwa ” mipango ya kuingilia na kupanua nchi ya Rwanda kamwe haitavumiliwa”.
Serikali ya Rwanda kwa mara kadhaa imekanusha tuhuma hizo za viongozi wa Kongo.
Katika tangazo lake, Rwanda imekariri ahadi yake ya kutaka suluhu ya usalama na utulivu kupitia jukwa la kikanda licha ya uchokozi wa FARDC ( jeshi la jumuhuri ya kidemokrasia ya Kongo)
Hadi wakati huu, kundi la M23 linadhibiti mji wa mpakani wa Bunagana tangu tarehe 13 juni mwaka huu pamoja na maeneo mengi ya wilaya ya Rutshuru katika mkoa wa kivu ya kaskazini mashariki mwa Kongo.
About author
You might also like
Kirundo: death threats against those who oppose forced contributions in Ntega commune
Residents of the Murungurira zone, Ntega commune, who have not agreed to pay the contribution demanded by the commune administrator and the communal secretary of the CNDD-FDD party are all
Burundi : the CNL party blocked by the Ministry of the Interior in its attempt to resolve its internal crisis
The president and legal representative of the CNL party sent a letter to the Burundian Minister of the Interior on February 26. Agathon Rwasa informed the minister that he is
Rumonge: two men including a CNDD-FDD official sentenced for outrage on authority
Both people are from Mutambara hill in the Gatete zone, in the commune and province of Rumonge (southwest of Burundi). They were among others, convicted for outrage on authority after