Kivu-kaskazini : vijiji vyasalia pasina wakaazi

Kivu-kaskazini : vijiji vyasalia pasina wakaazi

Vijiji vingi katika eneo la Jomba wilaya ya Rutshuru mkoa wa Kivu kaskazini mashariki mwa DRC vimesabaki pasina wakaazi kutokana na mapigano kuibuka tena alhamisi kati ya jeshi la FARDC na kundi la M23. Vyanzo eneo hilo vinaarifu kuwa watu wanakimbilia hasa nchini Uganda na kwenye vituo ambako wanaona usalama ni wa hakika. HABARI SOS Médias Burundi

Viongozi tawala wanaeleza kuwa familia kutoka eneo la Ntamugenga na Tarika wanaendelea kuwasili eneo la Rubare mji ambao uko karibu na makao makuu ya Rutshuru.

Wakati huo huo, wakaazi wa maeneo ya kibanda na Rangira wanakwenda kwa wingi kwenye makao makuu ya wilaya ya Rutshuru.

Wakaazi wa Tchengerero na Kabindi wanakimbilia Bunagana na wengi wamevuka mpaka na kuingia nchini Uganda.

Hali ni hiyo pia kwa wakaazi wa Bunagana wanaokimbia eneo hilo la mpakani na kupata hifadhi nchini Uganda.

Wananchi waliokimbilia nchini Uganda walipelekwa katika kambi ya Nakivale, mbali na mpaka.

Jeshi la FARDC ( jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) linaendelea kutuhumu kundi la M23 kuanzisha mapigano kwa lengo la kuzuia nenda rudi kwenye barabara kuu inayotumiwa kupeleka misaada kwa jeshi katika ukanda huo wakati ambapo waasi upande wao wanasema ni jeshi la FARDC lililoshambulia ngome zake na hivyo wakalazimika kujihami.

Previous North-Kivu: villages are emptying of their populations
Next Rwanda-DRC: DRC imetuhumu kwa mara nyingine Rwanda kusaidia kundi la M23 (tangazo)