Bubanza: vijana Imbonerakure 3 wamepinga kuripoti mbele ya askali polisi wa kupeleleza makosa

Bubanza: vijana Imbonerakure 3 wamepinga kuripoti mbele ya askali polisi wa kupeleleza makosa

Wanafunzi 3 wa shule ya Bubanza (ETB), wafuasi wa tawi la vijana Imbonerakure (Wajumbe wa tawi la vijana wa chama cha CNDD-FDD) wamepinga kuripoti mbele ya polisi wa upelelezi wa makosa ya jinai wa kamisha ya polisi tarafa ya Bubanza (magharibi mwa Burundi). Ni katika kesi ya kumpiga mwanafunzi mwingine. Wazazi walipeleka mashtaka dhidi ya vijana hao Imbonerakure walioshambulia mtoto wao hadi akalazwa hospitali. HABARI SOS Médias Burundi.

Misigaro Yves mwanafunzi katika mwaka wa pili shule ya ufundi wa magari, Soneramana Salomon wa mwaka wa pili wa ufundi wa kumpyuta na Mpawenayo Innocent wa mwaka wa tatu wa ufundi wa sayansi, wametakiwa kuripoti alhamisi hii kwenye kamishena ya polisi kujibu mashtaka dhidi yao ya kumpiga Fabrice Iteriteka mwanafunzi katika mwaka wa kwanza wa ufundi wa umeme.

Kisa hicho kilitokea usiku wa jumatatu wakati Iteriteka alikuwa katika mabweni akiwa mgonjwa. Begi ya mwanafunzi mmoja ilikuwa imeibiwa.

Wanafunzi-Imbonerakure hao waliohusika wana majukumu tofauti kwenye shule hiyo : Mmoja anahusika na mabweni, mwingine na usalama, wa tatu akitizama usafi kwenye shule hiyo.

” Walinipiga kwa zaidi ya masaa matano. Walimwaga maji kwenye viungo ambapo walinipiga kwenye mgongo na makalio. Siwezi kukaa ” aliwaambia wanafunzi wenzake muathiriwa huyo.

” Walimfunga mdomo na kitambaa ili kumuzuia kupiga kelele”, alitoa ushuhuda baba yake ambaye jumatano hii alikwenda kumujulia hali kijana wake.

” Nitatoa mashtaka ili wanafunzi hao waweze kuadhibiwa na kutoa fidia,” alisema baba wa muathiriwa.

Muhanga analia sana maumivu. Ana dalili za mtu aliyefanyiwa ukatili kwenye makalio yake na mgongo.

” Wana mazoea ya kupiga wanafunzi wengine bila kuchukuliwa hatua na viongozi wa shule. Tunaweza kusema kuwa ni watu wasioguswa”, wanalaani baadhi ya waalimu kwenye shule hiyo ya mabweni.

” Wanafunzi hao wana pia zaba za kijeshi ndani ya mabweni, mipira ya kuvaa na viatu ambavyo wanaonyesha wakati wakiwanyanyasa wanafunzi wengine” wanahakikisha walimu kwenye shule hiyo.

” Hujuwi sisi ni watu gani” walisema wakati wakimunyanyasa muhanga huyo.
” Kwingine wanafunzi kama hao wangekuwa wamefukuzwa tayari” analalamika mwalimu mmoja.

Viongozi wa shule wanafahamu hali hiyo. Wanataka kupuzia kisa hicho, vinaarifu vyanzo vyetu.

Lakini wazazi wa muhanga huyo wameamuru kuendelea na kesi hiyo ili wanafunzi hao waadhibiwe kwa mjibu wa sheria ya nchi na zile za ndani za shule hazikufanya kazi hasa kwa kesi ya wanafunzi hao watatu.
Vijana Imbonerakure wanatisha kwenye shule ya ETB kulingana na waalimu.

Siku ya alhamisi, vijana hao watatu wafuasi wa tawi la vijana wa chama cha CNDD-FDD walipinga kuripoti mbele ya polisi ya upelelezi ambayo iliwaitisha ili kujibu mashtaka dhidi yao, vyanzo vya polisi vilithibitisha hayo.

Katika maeneo mengi ya nchi hiyo ya afrika mashariki, vijana wafuasi wa chama tawala cha CNDD-FDD wanaendelea kujipa majukumu ya polisi na vyombo vya sheria licha ya baadhi kuwaadhibiwa tangu ujio wa utawala wa rais Neva .

Baadhi ya wadadisi wanasema kuwa wanaendelea kunufaika na hali ya kutoadhibiwa kama ilivyokuwa katika utawala wa Pierre Nkurunziza hali iliyopelekea umoja wa mataifa kuwaona kama kundi la silaha.

Previous Kivu-kaskazini: Jeshi na kundi la M23 wanapigana eneo la Rutshuru karibu na RN2
Next Ituri: five corpses discovered in the village of Mabiti