DRC: jamii ya kimataifa yafumbia macho vurugu zinazowakabili wananchi wa Kongo (Baba mtakatifu François)

DRC: jamii ya kimataifa yafumbia macho vurugu zinazowakabili wananchi wa Kongo (Baba mtakatifu François)

Baba mtakatifu François jumanne hii tarehe 31 januari alianza rasmi ziara ya siku sita barani Afrika. Anataraji kufanya siku nne nchini DRC na kumalizia siku zinazosalia nchini Sudan kusini. Alilaani ” ukoloni wa kiuchumi” unaoikabili nchi hiyo kubwa ya Afrika ya kati. Baba mtakatifu alituhumu pia jamii ya kimataifa kujiuzuru na kufumbia macho vurugu zinazowameza raia wa Kongo. HABARI SOS Médias Burundi

Mara baada ya kuwasili katika mji mkuu wa nchi hiyo yenye utajiri wa madini, baba mtakatifu alikutana na viongozi tawala, wajumbe wa mashirika ya kiraia na wanadiplomasia wanaofanyia kazi mjini Kinshasa. Alilaani uporaji dhidi ya DRC na Afrika .

[…], Inaumuza kuona maeneo haya hususan bara la Afrika likikabiliwa na aina mbali mbali ya manyanyaso….Afrika inatakiwa kutunzwa…Hali hiyo inatisha. Baada ya ukoloni wa kisiasa, ukoloni wa kiuchumi unaokamuwa yote ulifuata. Nchi hii ambayo inaporwa sana haijaweza kunufaika vya kutosha na rasilimali zake” alikisoa baba mtakatifu François mbele ya umati mkubwa unaomusikiliza.

Na kulaani ” tumefikia hali ya kukanganya ambapo matunda ya ardhi yake huwafanya wananchi wake kuwa kama wageni. Sumu ya uchoyo imesababisha umwagaji damu wa wananchi “.

Baba mtakatifu analinganisha hali nchini RDC kama ” janga ambalo mbele yake nchi zilizoendelea kiuchumi hufumbia macho, masikio na mdomo”. Kwa mtazamo wake, ” Kongo inatakiwa kusikilizwa, inahitaji nafasi na uangalifu”.

” Ondoweni mikono yenu nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, ondoweni mikono yenu barani Afrika. Sio mgodi wa kutumiwa, wala ardhi ya kuharibiwa, alisisitiza, na kupendekeza kuwa Afrika iweze kuwa mtetezi wa hatma yake.

Kujiuzuru kwa jamii ya kimataifa

Mkuu wa jiji la Vatican alikosoa vikali jamii ya kimataifa.

” Ukiangalia wananchi hao, unadhani kuwa jamii ya kimataifa ni kama vile ilijiuzulu na kufumbia macho vurugu zinazowameza. Hatuwezi kuzoea damu inayomwagika katika nchi hii kwa miongo kadhaa na kusababisha vifo vya ma elfu ya wananchi huku wengi wakiwa hawafahamu hali hiyo. Ni budi kupinga hali hiyo inayoendelea , mchakato wa amani unaoendelea na ambao ninaunga mkono kwa nguvu zote ni budi uungwe mkono katika hatua zake na ahadi zitekelezwe, alizidi kusema.

Aliwatolea mwito viongozi wa nchi hiyo kubwa ya Afrika ya kati kuwajari na kuwahudumia wananchi.

” Ambaye alipewa majukumu ya utawala anatakiwa kutenda kwa uwazi kwa kuzingatia majukumu aliyopewa kama njia ya kuhudumia jamii “, alikumbusha baba François kuhakikisha kuwa ” utawala unapata nafasi yake iwapo unatoa huduma”.

Na kusisitiza juu ya umuhimu ya ” kutenda katika muongozo huo na kujitenda na utawala wa kimabavu, kutafuta mali kwa urahisi na kiwi cha kupata pesa”. Mtume Paul anataja mambo hayo matatu kama ” mzizi wa maovu yote”.

Uchaguzi

Katika hutba yake ambayo alitoa akiwa amekaa kwenye kiti, mkuu huyo wa kanisa katoliki aligusia uchaguzi huku Kongo ikijiandaa kwa uchaguzi mwaka huu.

” Wakati huo huo, toa kipau mbele kwa uchaguzi huru, wa wazi unaoaminiwa na wote, kuwawezesha akinamama, vijana na makundi ya watu waliowekwa nyuma kushiriki katika mchakato wa amani, kutafuta amani na usalama wa wananchi kuliko maslahi ya watu au makundi ya watu na kuimarisha utawala kwenye ardhi yote ….” alifahamisha hayo.

Udanganyifu

” Tuache kudanganywa, au kununuliwa na wale wanaotaka nchi iweze kusalia katika vurugu kwa mantiki ya kujinufaisha na kufanya biashara ya aibu. Hali hiyo itasababisha aibu na fedheha pamoja na vifo na umasikini”.

Alilaani pia ” janga la kazi kwa watoto wadogo” na kuomba hali hiyo isimamishwe mara moja.

Baba mtakatifu analinganisha Kongo na madini ya almasi katika maumbile yake ambapo yanaonyesha ubora mkubwa wenye uwezo wa kunusurika dhidi ya kimikali lakini akatahadharisha kuwa ” mashambulizi ya mara kwa mara ya vurugu pamoja na hali za masikitiko zinaweza kudhofisha nguvu za raia wa Kongo, kupunguza nguvu za nafsi zao na kuwapelekea kupoteza matumaini na kujifungania katika hali ya majonzi”.

Baba François hatawasili mjini Goma( makao makuu ya Kivu-kaskazini ) kama ilivyokuwa imepangwa kabla. Lakini atawapokea wajumbe wa wahanga wa machafuko yaliyotendeka mashariki mwa Kongo.

Rais Félix Tshisekedi upande wake anasema ni ” mauwaji ya halaiki dhidi ya DRC yaliyopuzwa.

Baada ya DRC, baba mtakatifu ataelekea nchini Sudani kusini nchini nyingine iliyokumbwa na vita visivyoishi na mizozo ya kikabila.

Katika ziara yake nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo na Sudani kusini, baba François anataraji kutoa wito hadharani kwa viongozi wa mataifa hayo mawili kuchukuwa hatua dhahiri kwa ajili ya kumaliza hali ya kutoadhibu maovu yanayoadhibiwa na sheria ya kimataifa. Kuboresha hali ya uheshimishwaji wa haki za binadamu katika nchi hizo mbili haitawezekana bila jukumu la kuadhibu maovu yaliyotendeka wakati wa mzozo wa silaha”, alifahamisha Tigere Chagutah kiongozi wa eneo la Afrika mashariki na kusini wa shirika la Amnesty International.

Previous Nyarugusu : yafungwa maduka ya dawa yasiyojulikana
Next Rumonge : wakuu wapya wa tarafa bado kuanza rasmi jukumu lao. Huduma zinajikokota