Nyarugusu : yafungwa maduka ya dawa yasiyojulikana

Nyarugusu : yafungwa maduka ya dawa yasiyojulikana

Uwindaji wa wamiliki wa maduka ya dawa yasiyokuwa halali ulianzishwa ndani ya Nyarugusu. Shirika la Medical Team International linalohusika na sekta ya afya lina mpango wa kukataza tabia ya kujitibu na kujipangia dawa. HABARI SOS médias Burundi

Polisi, watu wanaojitolea, viongozi tawala pamoja na wahudumu walijumulishwa kuwahamasisha watu kuachana na tabia ya kujitibu wenyewe. Maduka na vibanda ambako dawa hununuliwa yalifichuliwa na kufungwa.

” Kisa cha kuchukulia mfano huo ni duka la dawa kubwa katika zone 9. Lilikuwa kwenye makaazi ya mkimbizi mmoja kutoka Burundi. Polisi imechukuwa madawa yote. Mumiliki wa duka hilo na mtumishi wamekamatwa. Nyumba iliyochukuliwa kama duka la dawa imefungwa” amethibitisha mkaazi wa zone hiyo.

Maduka ya dawa yamechukuliwa kama mahala pa kutibu na kupewa huduma za awali.

” Tulishuhudia kwa mfano vitongi vilivyokuwa vikiuzishwa karibu na nafaka za chakula, na watu wanaonunua dawa bila kuandikwa na muganga, etc…..Baya zaidi tulimukuta mgonjwa akipewa dawa kupitia serimu kati ya moja kati ya maduka ya madawa haliyofungwa. “Ni hali isoyovumilika ” walifafanua wahudumu wa shirika la Medical Team International.

Wito ulitolewa kwa kila mkimbizi anayejihisi vibaya kujielekeza kwenye kituo cha afya halali.

MTI hivi karibu ilichukuwa nafasi ya Croix Rouge katika sekta ya afya. Shirika hilo linataka kuleta mabadiliko ambayo kulingana na shirika ni kuongeza ubora wa huduma na kuhakikisha uheshimishwaji wa haki ya afya kwa kila mkimbizi.

Kambi hiyo inawapa hifadhi wakimbizi zaidi ya laki moja na elfu 10 wakiwemo warundi elfu 50, wanaosalia wakiwa wenye asili ya Kongo.

Previous Faili-Ecocash: Hali inazidi kuwa mbaya zaidi
Next DRC: jamii ya kimataifa yafumbia macho vurugu zinazowakabili wananchi wa Kongo (Baba mtakatifu François)