Faili-Ecocash: Hali inazidi kuwa mbaya zaidi

Faili-Ecocash: Hali inazidi kuwa mbaya zaidi

Tangu kuvurugika kwa zoezi la kutuma na kupokea pesa kupitia huduma ya Ecocash, wananchi wamekuwa na wasi wasi. Wahudumu wakuu na wasaidizi wanakabiliwa na hali ngumu. Wanaomba benki kuu kuingilia kati. HABARI SOS Médias Burundi

Hali inazidi kuwa mbaya katika siku tano za kuvurugika kwa huduma ya Ecocash.

” Ninamfahamu muhudumu ambaye ana karibu milioni 50 ya pesa za kieletroniki. Atapata aje kitita hicho? Baya zaidi ni marufuku kuondoa milioni 15 kwa siku”, analaumu ajenti mkuu ambaye anafanyia kazi katika jiji kuu la kibiashara.

” Inaonekana kama vile benki kuu ya taifa BRB ilikuwa anafamu tatizo hilo wakati ilipotoa tangazo la kukataza watu kuondoa milioni 15 kwa siku. Ni kupitia mfumo upi tutaweza kufanya kazi kama wahudumu wakuu wakati ambapo kati ya wasaidizi wetu, kuna wale wanazidisha milioni hizo 15 kwa siku”, alizidi kusema.

Ujanja

Baadhi ya watoa huduma hiyo hukata hadi asilimia 10 ya kitita kilichoombwa na mteja wakidai kuwa hawafanyi kazi tena”. Tunapata faida ndogo kupitia njia hiyo”.

Mhudumu mmoja anaeleza kuwa Ecocash ilimpatia franka za Burundi laki tano tangu siku ya ijumaa wakati ambapo ana zaidi ya milioni 10 za kutolewa .

” Ninatakiwa kufanya ujanja ili niweze kuishi” alifichuwa.

Wahudumu wengine wanafanya ujanja, kwa kusaidiwa na wafanyakazi wa kampuni ya Econet katika huduma yake ya Ecocash ili waweze kupata pesa, na rushwa ndio mfumo unaotumika. Madhara yake yanawakumba watu wote ambao wana pesa inayotakiwa kuondolewa. Taarifa hizo zinathibitishwa na mfanyakazi wa EConet.

Watoa huduma pamoja na waajiri wa kampuni hiyo wanalaani huduma ya Lumicash mshindani mkali wa Ecocash.

” unapoweka pesa ndani ya simu yako, kwa sasa operesheni hiyo ni bure, wakati ambapo mwanzo huduma hiyo ilikuwa na gharama “, baadhi ya wahudumu wanatishia kuacha kufanya kazi na Lumicash.

Athari za kuvurugika kwa huduma ya Ecocash zimekuwa nyingi, ni mtandao uliokuwa ukitumiwa zaidi katika mfumo wa kutuma pesa kupitia simu nchini Burundi. Michango na ukusanyaji wa pesa hufanyika kupitia mtandao huo uliokuwa wa uhakika, pamoja pia na malipo kulingana na wahudumu wakuu.

Tangu tarehe 26 januari, mfumo wa Ecocash umeparanganyika . Ni matokeo ya hatua ya mamlaka ya kukusanya mapato (OBR) iliyochukuwa udhibiti wa akaunti za shirika hilo la mawasiliano ya simu za mkononi Econet Wireless yenye mfumo huo. Kwa mjibu wa ofisi hiyo, kampuni hiyo inadaiwa na serikali ya Burundi zaidi ya bilioni 88 sarafu za Burundi na zaidi ya milioni 44 dola za kimarekani.

Kwa kusubiri mwisho wa hali hiyo, pesa imesalia ndani ya simu za watu.

Previous DRC: the international community has resigned to the violence devouring the Congolese people (Pope Francis)
Next Nyarugusu : yafungwa maduka ya dawa yasiyojulikana