Rumonge : wakuu wapya wa tarafa bado kuanza rasmi jukumu lao. Huduma zinajikokota

Rumonge : wakuu wapya wa tarafa bado kuanza rasmi jukumu lao. Huduma zinajikokota

Wakaazi wa tarafa za Rumonge, Bugarama na Buyengero mkoani Rumonge (kusini magharibi mwa Burundi) wanasema kuwa hawana haki za kupata baadhi ya karatasi kwa zaidi ya mwezi mmoja. Wanaomba waanze kufanya kazi viongozi hao wapya waliochaguliwa hivi karibuni. HABARI SOS Médias Burundi

Karatasi zinazokosekana kutokana na hali hiyo ni pamoja na kadi ya uraia, karatasi za uthibitisho wa umiliki wa viwanja na zingine. Wakaazi hawana haki ya kupata huduma zinazotolewa moja kwa moja na mkuu wa tarafa.

Wananchi waliozungumza na SOS Médias Burundi walifahamisha kuwa kuwa wale wanaohitaji kadi za uraia, huwa wanakwenda kuzitafuta katika mikoa au tarafa ambazo ziko na wakuu wa tarafa.

Wananchi hao wanatolea mwito viongozi kwenye wizara ya mambo ya ndani kuwakabidhi mapema madaraka viongozi hao wawili waliochaguliwa hivi karibuni ili wananchi waweze kupata tena haki ya kupewa huduma wanazotaka.

Viongozi hao wapya wa tarafa Augustin Minani wa tarafa ya Rumonge, Jean Nduwimana wa tarafa ya Bugarama na mwingine wa tarafa ya Buyengero Étienne Havyarimana walichagukiwa na mabaraza ya tarafa zao tarehe 13, mwingine 14 na wa tatu tarehe 15 januari 2023.

Wakuu hao wapya wa tarafa waliwarejelea wale wa zamani wanaokabiliwa na tuhuma za ” wizi wa vifaa vya ujenzi wa shule ambavyo vilitolewa na ofisi ya rais wa jamuhuri.

Wawili kati yao, mkuu wa tarafa ya Bugarama Charles Karorero na Gratien Nduwayo wa tarafa ya Buyengero waliachiliwa huru kwa muda tarehe 7 disemba 2022.

Vyanzo katika idara ya sheria vilifahamisha kuwa walikiri makosa na kuahidi kurejesha vifaa walivyopora.

Mkuu wa zamani wa tarafa ya Rumonge Jérémie Bizimana upande wake anaendelea kuzuiliwa katika gereza kuu la Mpimba ndani ya jiji kuu la biashara la Bujumbura. Kulingana na vyanzo vyetu, anaendelea kukanusha tuhuma dhidi yake.

” Alisahawu kuwa aliwahi kumutumia ujumbe wa sauti mwendeshamashtaka mkuu wa Rumonge akimuomba kuingilia kati ili angalau aweze kufukuzwa kazi kuliko kupelekwa jela” chanzo chetu kinakumbuka.

Ni kutokana na ujumbe huo wa sauti ambao rais Ndayishimiye alizingatia katika ” kumuchafua ” hadharani .

Previous DRC: jamii ya kimataifa yafumbia macho vurugu zinazowakabili wananchi wa Kongo (Baba mtakatifu François)
Next Rumonge: the new municipal administrators have not yet taken office, services are idling