Burundi: CVR tume ya ukweli na maridhiano yapanga kuchapisha ripoti ya maovu ya 1885 hadi 1971

Burundi: CVR tume ya ukweli na maridhiano yapanga kuchapisha ripoti ya maovu ya 1885 hadi 1971

Ripoti hiyo itawekwa hadharani kabla ya mwaka huu kumaliza, alifahamisha kiongozi wa tume ya CVR Pierre Claver Ndayicariye. Amezidi kuwa tume anayoiongoza itachunguza jukumu la kanisa katoliki na wakoloni katika mauwaji ya 1972 na majanga mengine ya kabla. HABARI SOS Médias Burundi

Pierre Claver Ndayicariye amesema hayo katika mafunzo kwa wandishi wa habari wa ndani na ma kamishena wa CVR ( tume ya ukweli na maridhiano) yaliyofanyika tangu alhamisi hadi jumamosi katika jiji kuu la kisiasa la Gitega.

Amesema ni ripoti ambayo haijafichuliwa na yenye umuhimu mkubwa ” na bado haijaonyeshwa viongozi wa nchi.

Bwana Ndayicariye kwa mara nyingine ameyataja mauwaji ya 1972 yaliyosababisha idadi kubwa ya vifo kutoka jamii ya Bahutu kuliko watutsi kuwa ni “mauwaji ya halaiki dhidi ya wahutu nchini Burundi ingawa rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye alihakikisha kuwa ni mapema kutaja mauwaji mbali mbali yaliyofanyika nchini Burundi miaka iliyopita”.

Kiongozi wa tume hiyo yenye utata mwingi anathibitisha kuwa Watutsi wengi waliuwawa bila hata hivyo kutumia neno la mauwaji ya kibinadamu au ya kuangamiza kama anavyofanya kuhusu mauwaji ya wahutu.

Tume ya CVR ni kati ya taasisi zilizoundwa kupitia makubaliano ya amani na maridhiano ya Arusha ya mwaka 2000. Tume hiyo inakosolewa vikali ukilinganisha na tume zingine zilizoundwa.
Inakosolewa na mashirika ya kutetea haki za Watutsi ambao wanatuhumu tume hiyo kushughulishwa na mauwaji yaliyofanyika dhidi ya jamii ya wahutu kuliko watutsi.

Tarehe 20 disemba 2021, kiongozi huyo wa tume inayopingwa alitangaza kuwa mauwaji ya 1972 yaliyosababisha idadi kubwa ya raia jamii ya wahutu kufariki kuliko wa tutsi, ni mauwaji ya halaiki dhidi ya kabila la wahutu nchini Burundi “. Ilikuwa mbali na kuwasilisha awamu ya tatu ya ripoti ya hatua ya kwanza kwa mabaraza mawili ya bunge katika jiji kuu la biashara la Bujumbura. Lakini rais Evariste Ndayishimiye katika mwezi mei alifahamisha kuwa ni mapema kutangaza kuwa mauwaji ya mwaka wa 1972 yalikuwa mauwaji ya kuangamiza “.

Burundi ina makabila sawa na Rwanda jirani yake wa kaskazini ambapo yalifanyika mauwaji ya jenoside dhidi ya watutsi mwaka wa 1994 na kuidhinishwa na UN.

Nchini Burundi licha ya kutaja kuwa mauwaji ya 1972 yanayofahamika kama ” janga la 1972″ ni mauwaji ya halaiki dhidi ya jamii ya wahutu ambao idadi kubwa wako kwenye utawala kwa sasa, makabila hayo mawali yanapata tabu kukubaliana kuhusu mizozo iliyopelekea vifo nchini Burundi.

Hadi sasa, jamii ya watutsi wanakubaliana kuwa mauwaji ya watu wa jamii hiyo yaliyotokea baada ya kifo cha rais wa kwanza wa kabila la wahutu aliyechaguliwa kidemokrasia mwaka 1993 kuuwawa ni ” mauwaji ya halaiki dhidi ya watutsi”, jambo ambalo linamushughulisha kidogo bwana Ndayicariye na tume yake ambao walijizuia katika baadhi ya mikoa kuwasili katika maeneo ambako makaburi ya pamoja ya watutsi yaliripotiwa.

Previous DRC: kiongozi wa zamani wa waasi Jean Bosco Ntaganda ametumwa katika jela nchini ubelgiji
Next Rugombo: discovery of a corpse