DRC: kiongozi wa zamani wa waasi Jean Bosco Ntaganda ametumwa katika jela nchini ubelgiji

DRC: kiongozi wa zamani wa waasi Jean Bosco Ntaganda ametumwa katika jela nchini ubelgiji

Kulingana na mkataba wa mahakama ya kimataifa, mahabusu waliokatiwa kesi wanalazimika kutumikia kifungo chao katika nchi iliosaini mkataba wa Roma juu ya uundwaji wa ICC. Jean Bosco Ntaganda kiongozi wa zamani wa kivita nchini Kongo alipokelewa nchini Ubelgiji kwa ajili ya kutumikia kifungo chake cha miaka 30. HABARI SOS Médias Burundi

Mwendeshamashtaka mashtaka mkuu wa ICC, alifamisha jumatano hii kuwa kiongozi huyo wa zamani wa waasi nchini Kongo, Jean Bosco Ntaganda alielekezwa na kupokelewa katika ufalme wa ubelgiji ili kutumikia kifungo chake ndani ya gereza la Leuze-en-Hainaut.

” ICC inategemea msaada wa mataifa kwa ajili ya kutekeleza vifungo vya mahabusu wake na inaridhika na ushirikiano wa hiari wa serikali ya ubelgiji katika kesi hiyo”, alifahamisha Peter Lewis mwandishi wa kesi katika mahakama ya ICC. Hali hiyo inakwenda sawa na mkataba wa ICC ambao unapanga kuwa wafungwa waliokatiwa kesi na ICC wanatumikia kifungo katika nchi nyingine iliyochaguliwa na korti hiyo kati ya mataifa yaliyosaini mkataba wa Roma”.

Naibu mkuu huyo wa jeshi zamani aliyehusika na operesheni za kijeshi katika kundi la wapiganaji la wazalendo kwa ajili ya kukomboa Kongo (FPLC), Ntaganda alikatiwa kifungo cha miaka 30 jela ” mwezi novemba mwaka wa 2019. Alipatikana na makosa 18 ya uhalifu wa kivita na mauwaji ya kibinadamu yaliofanyika eneo la Ituri (mashariki mwa DRC) kati ya 2002-2003.

Alizuiliwa katika mahakama ya ICC mjini the Hague tangu machi 2013.

Bosco Ntaganda aliyefahamika kwa jina la ” Terminator ” kutokana na ukatili wake ni maarufu sana katika kanda ya maziwa makuu ya afrika.

Kutoka mauwaji ya halaiki dhidi ya Watutsi nchini Rwanda (1994) hadi katika kundi la waasi la M23 mashariki mwa DRC, kiongozi huyo wa kivita alikuwa na jukumu katika mizozo iliochana kanda hii na ukatili wake dhidi ya raia wa kawaida.

Tarehe 13 julai 2012, mahakama ya kimataifa ilitoa waranti wa kukamatwa kwake kwa tuhuma za kufanya uhalifu wa kivita na maovu dhidi ya binadamu. Alijisalimisha mwenyewe kwenye ubalozi wa Marekani mjini Kigali nchini Rwanda tarehe 18 machi mwaka wa 2013, kuepuka kuuwawa na mmoja kati ya wapiganaji wake.

Amekatiwa na mahakama hiyo ya kimataifa mwezi machi mwaka 2021 kifungo cha miaka 30 jela

Previous Kivu-kaskazini: mkutano kati ya M23 na FARDC
Next Burundi: CVR tume ya ukweli na maridhiano yapanga kuchapisha ripoti ya maovu ya 1885 hadi 1971