Kivu-kaskazini: mkutano kati ya M23 na FARDC

Kivu-kaskazini: mkutano kati ya M23 na FARDC

Kundi la M23 linafahamisha kuwa liliwapokea wajumbe wa jeshi la Kongo, wale wa Monusco (ujumbe wa umoja wa mataifa nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo), wale wa kikosi cha kikanda pamoja pia mchakato wa uhakiki wa shirika la CIRGL (kongamano la kimataifa la nchi za maziwa makuu) katika mkutano wa kimkakati ndani ya eneo la Nyiragongo. Ni katika wilaya ya Kibumba mkoa wa Kivu kaskazini mashariki mwa DRC. Lengo la mkutano huo ni kupunguza uhasama kati ya pande mbili. HABARI SOS Médias Burundi

Mazungumzo yalifanyika jumatatu tarehe 12 disemba katika eneo la Kibumba, mji ulio kwenye umbali wa kilometa 20 kutoka Goma, makao makuu ya mkoa wa Kivu kaskazini. Mkutano huo uliongozwa na jemedali Jeff Nyagah, kamanda wa kikosi cha kikanda pamoja na kanali Nzenze Imani wa M23.

Katika tangazo lililowekwa hadharani, uongozi wa M23 unakaribisha juhudi za viongozi wa kikanda kwa ajili ya kumaliza kwa amani mzozo unaoendelea nchini DRC”.

Kundi hilo la waasi linasema kuwa linasubiri mkutano mwingine ambao tarahe yake haikupangwa.

Mkutano huo wa kwanza ulifanyika wakati ambapo tangu mji wa mpakani wa Bunagana kudhibitiwa na kundi la M23 miezi sita iliyopita, serikali ya Kongo ilikuwa imekiri kuwa ” hakuna uwezekano wa kuzungumza na kundi la M23 ambalo linachukuliwa na serikali kama kundi la kigaidi”.

Siku chache zilizopita, mazungumzo yalifanyika mjini Nairobi nchini Kenya, waasi hao wakiwa hawakualikwa pamoja na makundi ya waasi ya Kongo.

Kinshasa iliendelea kulichukuwa kundi la M23 kama kundi la silaha la Rwanda, sababu ya mvutano kati ya mataifa hayo maziwa makuu ya afrika.

Hali ni ya usalama ni ya wasi wasi katika maeneo ya Rutshuru na Nyiragongo ambapo kundi la M23 linatuhumiwa na mashirika ya kiraia ya Kivu kaskazini kuwauwa watu 300 eneo la Kishishe na maeneo mengine.

Viongozi wa Kongo walisema idadi ya watu 272 waliuwawa na Monusco inasema ni watu 131.

Wakati waziri wa Kongo wa sheria akiwa tayari alipeleka mashtaka katika mahakama ya ICC ( mahakama ya kimataifa) kuhusu kesi hiyo na kuituhumu Rwanda pamoja na waasi hao kufanya mauwaji hayo, kundi hilo la zamani la kabila la watutsi ambalo lilichukuwa tena silaha mwishoni mwa mwaka wa 2021 linaendelea kuomba uchunguzi ufanyike ” na kukubali kuwa watu nane waliuwawa na risasi zilizopoteza shabaha.

Msemaji wa M23 hivi karibuni alihakikishia SOS Médias Burundi kuwa ” watu wengine waliouwawa walikuwa wapiganaji wa Mai-Mai na FDLR kwenye uwanja wa mapambano na kusisitiza kuwa ” watakuwa raia wa kawaida iwapo watatuonyesha vitambulisho vyao, mahala ambapo wanaishi na familia zao.

Previous Nduta (Tanzania): mashirika mengi ya misaada yanapanga kusimamisha shughuli zao
Next DRC: kiongozi wa zamani wa waasi Jean Bosco Ntaganda ametumwa katika jela nchini ubelgiji