Nduta (Tanzania): mashirika mengi ya misaada yanapanga kusimamisha shughuli zao

Nduta (Tanzania): mashirika mengi ya misaada yanapanga kusimamisha shughuli zao

Angalau mashirika makuu manne ya misaada yatasimamisha huduma zake kuanzia januari mwaka wa 2023. Yatasimamisha huduma kutokana na ukosefu wa fedha. HABARI SOS Médias Burundi

Mashirika ya misaada ambayo tayari yalifahamisha kuwa yatasimamisha huduma ni pamoja na Women’s Legal Aid Center ( WILAC) inayojihusisha na sekta ya sheria, PLAN International inayosaidia watoto wa chini ya miaka 18, HelpAge International inayojihusisha na watu wazima na walemavu na IRC inayoshughulikia unyanyasaji dhidi ya akinamama.

” Mashirika hayo hayatatoa tena huduma hapa kambini. Msiwe na wasi wasi, huduma na misaada iliyokuwa inatolewa na mashirika hayo, itatolewa na shirika jingine la Danish Refugee Council (DRC). Ni kama kupishana, hakuna kitakachobadilika”, alihakikisha mfanyakazi wa HCR ambayo inahusika na uratibu wa mashirika hayo kabla ya kufafanua kuwa ukosefu wa fedha ndio sababu ya kusimamisha shughuli.

Hata hivyo wakimbizi wanahofia madhara ya hatua hiyo.

” Vipi huduma zilizokuwa zikitolewa na mashirika manne na zitakuwa zikitolewa na shirika moja ?Ni jambo la kawaida kuwa ubora wa huduma utapungua. Harafu ni mashirika muhimu yanayofunga milango”, analalamila mkimbizi kutoka Burundi, akihofia vifo kutokea mnamo siku zijazo.

Usitishwaji wa huduma umepokelewa vibaya.

“Tumetelekezwa. Ni pia ni ujumbe mzito ambao tunapewa na Tanzania na HCR. Wanataka turudi nyumbani kwa hali zote. Na hayo ni baada ya ziara ya viongozi wa Burundi hapa”, aliendelea mkimbizi huyo kwa hasira.

Wanaomba HCR “kutoanguka katika mtego wa Burundi na Tanzania” , kinyume chake, “HCR itakubali matokeo”

Haijajulikana iwapo mashirika hayo yatasimamisha shughuli katika kambi ya Nyarugusu.

Tanzania ina jumla ya wakimbizi 126.000 kutoka Burundi

Previous Kirundo: more than 900 repatriated schoolchildren have dropped out of school
Next Kivu-kaskazini: mkutano kati ya M23 na FARDC