Burundi: rais Neva anawatuliza watuhumiwa wanaofuatiliwa na ICC

Burundi: rais Neva anawatuliza watuhumiwa wanaofuatiliwa na ICC

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye aliongoza kipindi chake maluum kinachofunga mwaka na kuzungumzia maswala muhimu. Kati ya hayo, ni matamshi ya hivi karibuni ya ICC (mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita) ambayo ilifahamisha nia yake ya kufuatia watuhumiwa wa maovu yaliyofanyika katika nchi hiyo ndogo ya afrika mashariki katika mwaka wa 2015. “Tuko na mahakama zenye uwezo wa kushughulikia wahalifu” alifahamisha. HABARI SOS Médias Burundi

Kila mwisho wa mwaka, rais wa Burundi anaongea na wandishi pamoja na raia. Wananchi wengi walijielekeza mkoani Kirundo (kaskazini mwa Burundi) ili kumufikishia kero zao na wandishi wa habari ili kumuuliza maswali. Kwa muda wa masaa matatu, rais wa Burundi alisikiliza na kutoa majibu, ilikuwa ijumaa tarehe 30 disemba.

” Kuhusiana na swala la ICC, ninataka kuwa wazi : kila kitu kinapangwa na sheria. Katika kipindi ambapo Burundi ilikuwa mjumbe wa mahakama hiyo, kuna mikataba iliyokuwa imesainiwa. Kila nchi ina haki ya kujiondoa kwenye mikataba hiyo sababu na kujiunga ni bila shinikizo. Kwa vile Burundi ilijiondoa kwenye mkataba huo, kama wanataka kufanya hivyo, watalazimika kutuonyesha sheria waliozingatia. Burundi sio tena mwanachama wa ICC na yanayofanyika kwenye mahakama hiyo hayatuhusu” alimujibu raia Neva mwandishi wa habari wa ndani.

Na kuhakikisha : Burundi sio ile ya zamani. Zamani mtu angefanya makosa na kusalia huru. Lakini kwa sasa wahalifu wanaadhibiwa. Hata warundi wanaojificha katika nchi zingine tunaendelea kuomba nchi hizo kuwatuletea ili kesi dhidi yao zishughulikiwe nchini Burundi. Taasisi za kimataifa haziwezi kuwajibika kwa niaba ya Burundi wakati ambapo tuko na mahakama zenye uwezo”.

Rais Neva anakiri kuwa iwapo raia wa Burundi atasimamishwa akiwa kwenye ardhi ya nchi yoyote, itakuwa ni tatizo kati ya nchi hiyo na Burundi sio kati ya Burundi na ICC “.

” Hata na sisi, tutakaposimamisha raia wa nchi nyingine, nchi hiyo inayo haki ya kuomba akabidhiwe nchi yake. Nafikiria kuwa iwapo kuna raia wa Burundi anayetuhumiwa kosa hili au lile, ni jukumu la Burundi kushughulikia kesi yake”, alibaini rais huyo ambaye siku huyo alimufuta kazi msemaji wake alikuwa amegeuka mtu asiyetabirika kulingana na vyanzo katika ikulu ya rais.

Tangu oktoba 2017, Burundi sio tena mwanachama wa mkataba wa Roma wa kuanzisha ICC.

Lakini hivi karibuni, mahakama hiyo ilifahamisha kuwa uchunguzi kuhusu Burundi unaendelea vizuri, na kwamba unaelekea kukamilika. Hatua ya kufuata ni waranti za kimataifa kutolewa dhidi ya watuhumiwa uhalifu.

Hayo ni wakati ikiwa ni miaka mitano baada ya uchunguzi kuhusu maovu yaliyotendeka nchini Burundi katika mzozo wa kisiasa wa 2015 kuanza. Mzozo huo ulisababishwa na muhula mwingine wa kutatanisha wa rais Pierre Nkurunziza.

Previous Mutaho: aliyefanya mauwaji ya mrasibu wa kituo cha posta ahukumiwa kifungo cha maisha jela
Next Rwanda-DRC: jamii ya kimataifa inasifu amani ya mdomoni (Paul Kagame)