Rwanda-DRC: jamii ya kimataifa inasifu amani ya mdomoni (Paul Kagame)

Rwanda-DRC: jamii ya kimataifa inasifu amani ya mdomoni (Paul Kagame)

Imekuwa mara ya kwanza kwa rais wa Paul Kagame kuchukuwa muda mrefu kwa ajili ya kuzungumzia hali ya nje ya nchi yake na kujieleza katika lugha ya kingereza wakati akihutubia hususan raia wa Rwanda. Alithibitisha kuwa kundi la FDLR lililofanya mauwaji ya halaiki nchini Rwanda limegeuka mshirika wa jeshi la FARDC (Jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) na kutaja kuwa hali hiyo haiwezi kukubaliwa na Rwanda. Katika hutba yake kwa taifa kukaribisha mwaka mpya wa 2023 ambayo alitoa siku ya jumamosi tarehe 31 disemba, rais wa Rwanda alituhumu sehemu ya jamii ya kimataifa kuendelea “kupendelea viongozi wa Kongo wakati ambapo wameshindwa kupata suluhu la mzozo wa usalama mashariki mwa Kongo baada ya kutumia ma bilioni ya dola za kimarekani”. Kwa mjibu wake, jamii ya kimataifa inasifu amani ya mdomoni. HABARI SOS Médias Burundi

Ili kufikisha ujumbe wake kwa jamii ya kimataifa inayoendelea kutuhumu nchi yake kuunga mkono kundi la M23, rais Paul Kagame alijieleza katika lugha ya kingereza katika sehemu kubwa ya hutba yake.

” Inakatisha tamaa kuona jamii ya kimataifa ikisifu amani ya mdomoni na mwishowe kuhatarisha mazingira ya mchakato wa amani wa kikanda”, alisema akiwa mtulivu.

Na kushambulia zaidi” baada ya kutumia ma dorzeni ya ma bilioni kwa ajili kurejesha amani katika miongo miwili iliyopita, hali ya usalama mashariki mwa Kongo ilizidi ni mbaya zaidi. Ili kuelezea juu ya kushindwa kumaliza tatizo hilo, baadhi ya wajumbe wa jamii ya kimataifa wanatuhumu Rwanda hata kama wanafahamu vizuri kuwa jukumu ni la serikali ya Kongo kwanza kabla ya washirika hao wa nje wanaoshindwa kushughulikia chanzo cha tatizo hilo kuliko chochote kingine”.

Kwa mjibu wa rais Kagame,” huo ni uongo wenye gharama isiokuwa na sababu yoyote”.

Kupendelea viongozi wa Kongo ili kulinda maslahi

Kulingana na rais wa Rwanda, jamii ya kimataifa inaendelea kupendelea viongozi wa Kongo kwa ajili ” ya kulinda maslahi”.

” Wanasema ukweli kwa kujificha kwa kuhofia kutofurahisha serikali ya Kongo na kupoteza maslahi yao. Lakini hakika wanawasaidia viongozi wa Kongo kuzidi kuchukuwa hatua za kuwapa moyo wananchi wa chini katika mchakato ambao unadanganya vibaya wananchi wao”, alizidi kusema.

Na kushindilia hivi ” hata kama kundi la wataam wa UN walionyesha ushirikiano wa jeshi la Kongo na kundi la FDLR na makundi mengine, bila kuzungumzia kauli ya chuki inayotia wasi wasi, habari hizo zilipuziwa kama vile hazina madhara”.

Kwa mjibu wa Bwana Kagame, mwenendo huo unavunja moyo na haukutarajiwa.

” Tumechoshwa na unafiki huo”, alisisitiza.

” Ni wakati mwakafa wa kuacha kusingizia nchi ya Rwanda” alibaini rais Kagame.

Rwanda kuathiriwa na hali ya mashariki mwa Kongo

Kwa mjibu wa Paul Kagame, nchi yake iliathiriwa na hali inayojiri mashariki mwa nchi hiyo kubwa ya afrika ya kati, jirani yake.

” Hakika tunaathiriwa moja kwa moja iwapo mabaki ya makundi yaliotekeleza mauwaji ya halaiki yamegeuka kikosi cha ushirika cha jeshi la DRC na kufanya mashambulizi ya kuvuka mipaka”, alizidi kuelezea.

Na kuendelea na kauli hiyo” hakuna hata nchi moja inayoweza kukubali hilo. Rwanda haitakubali kulichukulia swala hilo kama la kawaida na itajibu kama inavyotakiwa sababu usalama wetu na ustaawi ni kipau mbele “, na kukumbusha kuwa kuna zaidi ya makundi ya silaha mia moja mashariki mwa Kongo likiwemo kundi la waasi waliofanya mauwaji nchini Rwanda la FDLR.

” Makundi hayo yanakuwa chanzo cha usalama mdogo kwa raia wa kawaida nchini DRC na Rwanda. Hali hiyo inaendelea kwa sababu DRC haitaki au haina uwezo wa kutawala ardhi yake” alihakikisha Paul Kagame.

” Je, Rwanda inatakiwa kuvumilia uwendeshaji mbaya wa nchi hiyo kubwa? , alijiuliza.

Bila kujata jamii zao, alisikitishwa na hali ya wakimbizi kutoka Kongo ambao wanajikuta wakinyimwa haki yao ya msingi ya kupewa utaifa na nchi yao ya asili.

” Sio tu swala la ujumbe wa chuki lakini ni unyanyasaji unaoendelea kwa miongo” alikumbusha .

Bwana Kagame alifahamisha kuwa Rwanda ni kati ya nchi za jumuiya ya afrika mashariki iliyowapokea ma mia ya wakimbizi kutoka Kongo.

” Tulipokea zaidi ya wakimbizi elfu 70 nchini Rwanda peke. Na wengine wanaendelea kuwasili hadi sasa”, alihakikisha .

” Lakini jamii ya kimataifa inaendelea kukanusha kuwa watu hao hawajawahi kuwepo….Mpango wao ni watu hao kubakia daima nchini Rwanda, msimamo ambao utasaidia kuimarisha uongo ambao unasema ni raia wa Rwanda wanaotakiwa kufukuzwa.Hilo ni tatizo la kimataifa linalotakiwa kupatiwa jibu la kimataifa “, alishambulia rais wa Rwanda.

” Rwanda haitakubali kubeba mzigo wa viongozi wa DRC. Tuna mizigo yetu ya kubeba ambayo ni ya kutosha “, alimalizia .

Viongozi wa Kongo hawajajieleza kuhusu kauli hiyo ya rais wa nchi hiyo ya Rwanda.

Lakini jumanne iliyopita, waliwatambulisha watu wawili wenye asili ya Rwanda kwa vyombo vya habari wafanyakazi katika shirika la afrika kwa ajili ya maendeleo ya afya na kuwataja kama ” wapelelezi” ambao walikuwa wakipanga ” kuangusha ndege ya rais wa Kongo Félix Tshisekedi”.

Uhusiano kati ya hizo nchi mbili za maziwa makuu ya afrika unazidi kuzorota tangu kuibuka tena kwa kundi la machi 23, kundi la M23.

Kundi hilo la watutsi lililochukuwa tena silaha mwishoni mwa mwaka wa 2021 linatuhumu viongozi wa Kongo kushindwa kutekeleza ahadi zake kuhusu kuwarejesha katika maisha ya kawaida wapiganaji wake ambao ni raia wa jamii ya Batutsi wa Kongo.

Viongozi wa Kongo wanakubaliana kuwa kundi hilo linatapa usaidizi kutoka Rwanda, hali ambayo serikali ya Rwanda inatupilia mbali.

Baada ya kuchukuwa udhibiti wa maeneo mengi ya mkoa wa Kivu-kaskazini mashariki mwa DRC likiwemo la Bunagana, mji wa mpakani na Uganda na kutishia kuchukuwa udhibiti wa mji wa Goma makao makuu ya Kivu kaskazini mwishoni mwa juni iliyopita, waasi wa M23 waliachia kikosi cha kanda ya EAC ngome zake za Kibumba, disemba 2022.

Serikali ya Kongo hivi karibuni ilituhumu kundi hilo kufanya mauwaji ya raia 272 katika vijiji viwili chini ya udhibiti wa kundi hilo huku UN ikisema ni watu 130 waliouwawa.

M23 ilipinga madai hayo na kuyataja kama ” propaganda yenye nia ya kuchafua kundi hilo mbele ya wananchi” na kuomba uchunguzi huru ufanyike.

Rwanda upande wake daima ilituhumu FARDC (jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) kushirikiana na kundi la FDLR la waliofanya mauwaji ya halaiki kwa lengo la kusambaratisha nchi hiyo”

Lakini rais wa Kongo kwa mara kadhaa, alimutuhumu mwenzake wa Rwanda Paul Kagame kuunga mkono waasi na kuzidi kuwa ” kundi la FDLR sio tena tishio kwa Rwanda na kulitaja kama kundi lililopungukiwa na nguvu ou kundi la wezi”.

Previous Burundi: rais Neva anawatuliza watuhumiwa wanaofuatiliwa na ICC
Next Bujumbura: mripuko wa maradhi ya kipindupindu