Bujumbura: mripuko wa maradhi ya kipindupindu

Bujumbura: mripuko wa maradhi ya kipindupindu

Takriban watu 17 walipatikana na ugongwa wa Kipindupindu katika tarafa ya Kinama (kaskazini mwa jiji la biashara la Bujumbura) kulingana na waakazi. Wanahakikisha kuwa watu wawili tayari walifariki dunia. Ni visa vilivyoshuhudiwa tangu 30 disemba iliyopita. Waziri wa afya pamoja na muakilishi wa shirika la afya duniani OMS waliwasili jumapili hii katika tarafa hiyo ili kushuhudia hali hiyo. Mripuko wa ugonjwa wa kipindupindu ulitangazwa. HABARI SOS Médias Burundi

Waakazi wa tarafa ya Kinama wanafahamisha kuwa wanapata usumbufu wa kupata maji safi na vyoo vya viwango.

” Baadhi ya kata za karibu na tarafa ya Buterere wanashuhudia uchafu kutoka eneo la kata za Cibitoke na Mutakura ukimiminika katika maeneo ya tarafa hiyo. Ukosefu wa mifereji ni chanzo cha hali hiyo” wakaazi wanaeleza.

Jumapili iliyopita, ujumbe unaoongozwa na waziri wa afya na mjumbe wa shirika la afya duniani OMS (WHO) nchini Burundi waliwasili kushuhudia hali hiyo.

Waziri wa afya Daktari Sylvie Nzeyimana alitangaza kuwa eneo la kaskazini mwa jiji kuu la biashara linakabiliwa na mripuko wa visa vya ugonjwa wa kipindupindu . Alikiri kuwa visa 12 vya maradhi hayo vilipatikana wakiwemo watu 5 ambao tayari walipona na 7 wengine bado wanalazwa kwenye hospitali ya Prince Régent Charles (kati kati mwa jiji la Bujumbura)

Kupitia tangazo lililosomwa kwenye radio na Televisheni vya Burundi, alitangaza eneo la kaskazini mwa jiji la Bujumbura kuwa linakabiliwa mripuko wa ugonjwa huo wa kipindupindu.

Katika maeneo hayo, shughuli za kunyunyizia dawa majumba na vyoo katika familia zilizoshuhudia visa vya maradhi hayo ziliendeshwa jumapili hii na shirika la msalaba mwekundu nchini Burundi pamoja pia na ugaji wa maji safi

Previous Rwanda-DRC: jamii ya kimataifa inasifu amani ya mdomoni (Paul Kagame)
Next Mutaho: the alleged murder of the Régie Nationale des Postes' manager received a life sentenced