Mutaho: aliyefanya mauwaji ya mrasibu wa kituo cha posta ahukumiwa kifungo cha maisha jela

Mutaho: aliyefanya mauwaji ya mrasibu wa kituo cha posta ahukumiwa kifungo cha maisha jela

Katika kesi ya mafumanio mbele ya chumba cha uhalifu cha mahakama kuu ya Gitega (mji mkuu wa kisiasa) jumamosi hii, Chadrack Irakoze (miaka 30) alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la mauwaji ya kukusudia dhidi ya mrasibu mkuu wa kituo cha posta tarafani Mutaho Emmanuel Ndayizeye mwenye umri wa miaka 50. Muhanga aliuwawa kwa kupigwa risasi siku ya ijumaa akiwa ofisini mwake tarafani Mutaho mkoa wa Gitega (kati kati mwa Burundi). HABARI SOS Médias Burundi

Dereva huyo na pia fundi mekanika mkaazi wa kijiji cha Bihororo tarafa ya Giheta( Gitega) alikiri kosa bila hata hivyo kueleza sababu za kufanya mauwaji hayo.

” Hakupora hata pesa. Hakika ni muuwaji aliyepewa jukumu la kumumalizia maisha muhanga”, alibaini mtu mmoja aliyesikikiza kesi hiyo.

Chadrack Irakoze alifahamisha kuwa alinunua silaha iliyofanya mauwaji hayo nchini jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo kwa ajili ya kijilinda.

Mwendeshamashtaka ya jamuhuri aliomba muhusika wa mauwaji hayo apewe adhabu ya kifungo cha maisha jela. Muhusika aliomba adhabu hiyo ipunguzwe.

Baada ya kutathmini majaji waliamuru apewe adhabu ya kifungo cha maisha jela.

Previous Rwanda-DRC: tuhuma za DRC kuwa Rwanda inafanya upelelezi dhidi yake ni ongezeko la vishawishi kwa wananchi kushambulia
Next Burundi: rais Neva anawatuliza watuhumiwa wanaofuatiliwa na ICC