Rwanda-DRC: tuhuma za DRC kuwa Rwanda inafanya upelelezi dhidi yake ni ongezeko la vishawishi kwa wananchi kushambulia

Rwanda-DRC: tuhuma za DRC kuwa Rwanda inafanya upelelezi dhidi yake ni ongezeko la vishawishi kwa wananchi kushambulia

Ofisi ya msemaji wa serikali ya Rwanda ilitoa tangazo ambamo inasema kuwa kisa cha kuwafunga wananchi wa Rwanda wawili katika mji mkuu wa Kongo kwa tuhuma za kufanya ujasusi ni ishara ya ongezeko la vishawishi kwa wananchi kushambulia. Rwanda inatahadharisha pia kuhusu ujumbe wa chuki dhidi ya raia wanaozungumza Kinyarwanda wanaoishi nchini DRC. HABARI SOS Médias Burundi

Raia hao wenye asili ya Rwanda ambao ni daktari Juvenal Nshimiyimana na Moses Mushabe wote wawili wakiwa wafanyakazi wa shirika la afrika la maendeleo ya afya wanazuiliwa mjini Kinshasa tangu tarehe 30 agosti.

Kulingana na tangazo lililosainiwa tarehe 29 disemba, walionyeshwa kama ” wapelelezi” kupitia vyombo vya habari katika kikao cha jumanne tarehe 27 disemba 2022 mjini Kinshasa na naibu waziri wa Kongo wa mambo ya ndani Jean-Claude Molipe Mandongo.

” Siku chache tu baada ya kundi la watalaam wa UN kuonyesha ongezeko la mashambulizi na chuki za kikabila dhidi ya raia wa Rwanda, wanaozungumza Kinyarwanda na jamii ya watutsi wenye asili ya Kongo, zinazofanywa na viongozi wa Kongo, maafisa wakuu wa jeshi na viongozi wa mashirika ya kiraia, kikao na wandishi wa habari kilichoongozwa jumanne hii na naibu waziri wa mambo ya ndani kilionyesha ongezeko la hisia za ubaguzi na vishawishi kwa raia kufanya mashambulizi”, tangazo hilo linafahamisha.

Kulingana na tamko hilo, Rwanda inasikilishwa na hatma ya raia wake hao wawili wanaozuiliwa mjini Kinshasa tangu agosti 30 mwaka wa 2022 ambao walitambulishwa kama ” majasusi” kwa vyombo vya habari.

” Viongozi ambao wameshindwa kuwajibika au kukubali makosa yao, huwa wanajihusisha na kushawishi watu kufanya ubaguzi wa kikabila na kutuhumu makosa watu wa nje iwapo kumetokea janga. Hakuna mtu wa kanda ya maziwa makuu asiyejuwa wapi vitendo hivyo vinapeleka watu” tangazo hilo linaendelea kusema.

Katika kikao hicho na wandishi wa habari, viongozi wa Kongo walihakikisha kuwa raia hao wawili wanaozuiliwa walikuwa wanatayarisha kuangusha ndege ya rais wa Kongo wakichukulia mfano wa yaliyofanyika wakati wa mauwaji ya halaiki nchini Rwanda” , tangazo hilo linafamisha .

” Tunaomba viongozi wa DRC kuachana na kauli ya chuki na kuacha njia hiyo wanayoonekana kuchukuwa. Jamii ya kimataifa wakiwemo hao wanaojizuia kukosoa viongozi wa Kongo, wangetakiwa kuzingatia hayo na kuwajibishwa viongozi wa DRC kuhusu jukumu lao katika kuongeza chuki” linamaliza tangazo hilo.

Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ya maziwa makuu ya afrika unazidi kuzorota tangu kuibuka tena kwa kundi la machi 23, M23.

Kundi hilo la waasi wa kitutsi lilichukuwa tena silaha mwishoni mwa mwaka wa 2021 na kutuhumu viongozi wa Kongo kutoheshimu ahadi zake kuhusu kurejesha katika maisha ya kawaida wapiganaji wake ambao ni watutsi wa Kongo.

Viongozi wa Kongo wanaendelea kukiri kuwa kundi hilo linaungwa mkono na Rwanda, jambo ambalo serikali ya Rwanda inatupilia mbali.

Baada ya kuchukuwa udhibiti wa maeneo mengi ya mkoa wa Kivu-kaskazini mashariki mwa DRC likiwemo eneo la Bunagana, mji wa mpakani na Uganda na kutishia kukamata makao makuu ya mkoa wa Kivu-kaskazini tangu juni iliyopita, waasi wa M23 waliachia ngome zake za Kibumba ( wilaya ya Nyiragongo) kwa kikosi cha kanda ya EAC wiki moja iliyopita.

Serikali ya Kongo hivi karibuni ilituhumu kundi hilo kufanya mauwaji ya watu 272 raia wa kawaida katika vijiji viwili chini ya udhibiti wake, huku UN ikisema ni watu 130 waliouwawa.

M23 ilipinga madai hayo na kuyataja kama ” propaganda ” inayolenga kuchafua sura ya kundi hilo mbele ya wananchi” na kuomba uchunguzi huru ufanyike.

Rwanda upande wake, iliendelea kutuhumu FARDC ( jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) ” kushirikiana na kundi la waliofanya mauwaji ya kimbari nchini Rwanda la FDLR kwa lengo la kusambaratisha nchi hiyo”.

Lakini rais wa Kongo Félix Tshisekedi kwa mara nyingi alituhumu mwenzake wa Rwanda Paul Kagame kuunga mkono waasi hao na kudai kuwa ” kundi la FDLR sio tishio tena kwa Rwanda na kulitaja kama kundi dogo ambalo liligeuka kundi la majambazi”.

Previous Minembwe: the Congolese army and the Twirwaneho armed group have lost 11 elements
Next Mutaho: aliyefanya mauwaji ya mrasibu wa kituo cha posta ahukumiwa kifungo cha maisha jela