Burundi : shirikisho la vyama viwili vya kutetea haki za wafanyakazi vinaomba CNDS kuingilia kati katika mzozo dhidi ya serikali

Burundi : shirikisho la vyama viwili vya kutetea haki za wafanyakazi vinaomba CNDS kuingilia kati katika mzozo dhidi ya serikali

Mashirikisho ya vyama vya wafanyakazi COSYBU na CSB vinapaza sauti dhidi ya kusimamishwa kwa tozo za michango ya wajumbe wao. Serikali iliweka hatua ya kupiga marufuku michango ya wajumbe wa vyama vya wafanyakazi kuchukuliwa moja kwa moja kwenye mishahara yao. Mashirika hayo mawili yanaomba upatanishi wa kamati ya kitaifa ya mjadala wa kijamii (CNDS) ufanyike kuhusu swala hilo. HABARI SOS Médias Burundi

Kupitia malalamiko dhidi ya serikali ya Burundi yaliyowasilishwa kwa mkuu wa kamati ya kitaifa ya mjadala wa kijamii, shirikisho la vyama vya wafanyakazi COSYBU na CSB vinatoa wito, kwa niaba ya vyama vyote vya kutetea haki za wafanyakazi nchini i Burundi kwa CNDS kuunganisha pande mbili kuhusu swala la hatua ya serikali ya kusimamisha michango kuwa ilitolewa moja kwa moja kwenye mishahara ya wajumbe wa vyama hivyo.

Mashirikisho hayo mawili yanathibitisha kuwa hatua hiyo inazorotesha urasibu mzuri wa ofisi zao.

Mashirika hayo mawili yanatuhumu serikali kukiuka sheria kuhusiana na utekelezwaji wa makubaliano 87 ya OIT ( shirika la kimataifa kuhusu kazi) kuhusu uhuru wa kuunda chama cha wafanyakazi na kulinda haki ya kuunda chama cha wafanyakazi pamoja pia na makubaliano nambari 135 kuhusu kuwalinda wawakilishi wa wafanyakazi na kuwarahisishia.

Katika ziara za wajumbe wa serikali zilizofanyika kati ya januari na februari mwaka huu, waziri mkuu Gervais Ndirakobuca akiwa mkoani Makamba, alifahamisha kuwa hatua ya kutoa tozo ya michango moja kwa moja kwenye mishahara kwa ajili ya vyama vya wafanyakazi imesimamishwa.

Baadhi ya wafanyakazi walilaani kuona kuna kiwango cha pesa kilichokatwa kwenye mishahara kufadhili vyama vya ushirika ambapo sio wajumbe.

Kupitia mashtaka hayo yaliyowasilishwa tarehe 4 aprili 2023, shirikisho la vyama vya ushirika la COSYBU na CSB, hawajapinga kuwepo kwa visa vya aina hiyo lakini wanaitumu serikali kuharakisha kuchukuwa hatua ya kusitisha tozo hilo badala ya kujadili na wawakilishi wa vyama vya ushirika ili kuonyesha majukumu ya kila upande.

Mashirika hayo yanaomba mazungumzo yafanyike kumaliza mara mwisho swala kuhusu haki ya kujiunga na chama cha ushirika utekelezwaje.

Previous Goma: mahakama ya kijeshi yaahirisha kesi ya kigogo wa Lucha
Next DRC : sheria kuhusu uhuru wa vyombo vya habari inataraji kutangazwa

You might also like

Jamii

Mgogoro wa kijamii Burunga: batwa waomba msaada zaidi wa kuokoa shule na kuishi kwa familia

SOS Médias Burundi Burunga, Septemba 13, 2025 – Katika mkpa wa Burunga, kusini mwa Burundi, umaskini unazikumba familia za Wabatwa pakubwa: watoto wanaacha shule na akina mama wanageukia shughuli hatarishi

Jamii

Bujumbura: Wachuuzi wa mitaani – “Hatuishi tena, tunavumilia”

SOS Médias Burundi Bujumbura, Julai 29, 2025 – Wakikabiliwa na kupanda kwa bei, wanawake wachuuzi mitaani mjini Bujumbura, mji mkuu wa kiuchumi wa Burundi, wanatatizika kuishi. Biashara zao ndogo, injini

Haki

Gitega : hakuna sheria miaka 27 baada ya mauwaji ya askofu Joachim Ruhuna

Askofu Joachim Ruhuna mkuu zamani wa dayosezi ya Gitega aliuwawa tarehe 9 septemba 1996. Mauwaji hayo yalifanyika karibu na mto wa Mubarazi. Katika kipindi hicho, maeneo ya Bugendana na Mutaho