Ngozi : mfuasi wa chama cha CNL apatikana akiwa maiti
Muili wa Gilbert Ndacayisaba mwenye umri wa miaka 47 ulipatikana katika shamba la miti ya mikaratusi alhamisi mchana. Mkaazi huyo wa kijiji cha Karungura tarafani Mwumba mkoa wa Ngozi (Kaskazini mwa Burundi), alikuwa mmoja kati ya viongozi wa chama hicho cha upinzani katika eneo hilo. Watu wake wa karibu wanadai kuwa huenda aliuwawa na Imbonerakure (wajumbe wa tawi la vijana wa chama cha CNDD-FDD). Wawili kati ya Imbonerakure wanne wanaotuhumiwa mauwaji hayo walikamatwa. HABARI SOS Médias Burundi
Muili wake ulikuwa ndani ya mfuko wakati ulipogunduliwa na watoto waliokuwa wakitafuta kuuni za kupikia.
” Tuliona mfuko ambao ndani yake kulikuwa kitu. Tuliangalia na tukagundua kuwa ndani kuna maiti. Tulipata woga, tukatoa taarifa kwa wakaazi”, alieleza shahidi mmoja katika wale waliofanya ugunduzi huo wa kutisha.
Kwa mjibu wa mfuasi wa chama cha CNL katika kijiji hicho cha Karungura, marehemu alikuwa miongoni mwa viongozi wa chama hicho cha upinzani eneo hilo. Huenda aliuwawa kutokana na msimamo wake wa kisiasa.
” Mara nyingi alifanyiwa vitisho na Imbonerakure wa kijiji cha Karungura ambao nia yao walitaka ajiunge na chama tawala cha CNDD-FDD lakini bila kufanikiwa. Waliahidi hata kumupa adhabu. Hatukuamini kuwa wangefikia hata kumumalizia maisha”, walieleza wafuasi wa chama hicho.
Imbonerakure wawili walikamatwa, wawili wengine walikimbia. Wanatuhumiwa kuhusika na mauwaji hayo.
Waliokamatwa, wanazuiliwa katika kamishena ya polisi ya Mwumba.
Polisi inahakikisha kuwa uchunguzi unafanyika.
Gilbert Ndacayisaba alitoweka jumatano tarehe 6 aprili jioni wakati akielekea nyumbani kwake kwa mjibu wa watu wa karibu yake. Wanaomba ufanyike uchunguzi huru.
You might also like
Cibitoke: watu wanne waliuawa na viboko ndani ya mwezi mmoja
Watu wanaojihusisha na biashara haramu ya mafuta katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ili kuyaleta Burundi kupitia Mto Rusizi wako katika hatari ya kunyakuliwa na viboko. Tayari watu wanne wameuawa
Rumonge: Soko kuu lafungwa ili kulazimisha uondoaji wa kadi za wapiga kura
SOS Médias Burundi Rumonge, Mei 14, 2025 – Jumatano hii asubuhi, milango ya soko kuu la Rumonge (kusini-magharibi mwa Burundi) ilisalia imefungwa kwa saa kadhaa, kwa amri ya mamlaka ya
Wiki tatu baada ya Kufunguliwa tena, Barabara ya Uvira-Bukavu yakuwa korido ya kodi inayotozwa kwa watu.
SOS Médias Burundi Uvira, Aprili 21, 2026 – Wiki mbili baada ya kufunguliwa upya kwa Njia ya Kitaifa ya 5, inayounganisha jiji la Uvira na Bukavu katika jimbo la Kivu
