Ituri: watoto waangamia katika mashambulizi ya makundi ya silaha mkoani Ituri
Tangu disemba 2022, angalau watoto 60 waliuwawa katika vurugu za makundi ya silaha mkoani Ituri kaskazini mashariki mwa jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Takwimu hizo zilitolewa na ujumbe wa shirika la umoja wa mataifa kwa ajili ya amani nchini Kongo (MONUSCO) ofisi ya mkoa. HABARI SOS Médias Burundi
Takwimu hizo za kusikitisha zilitolewa wakati wa uzinduzi wa mazungumzo ya jamii ya Hema yanayofanyika eneo la Bunia tangu siku chache zilizopita.
Karna Soro, mkuu wa MONUSCO mkoani Ituri, anaeleza kuwa watoto hao ni kati ya wananchi 310 waliouwawa na vikundi vinavyotajwa kuwa vibaya tangu mwishoni mwa mwaka jana mkoani Ituri.
” Kati ya tarehe mosi disemba 2022 na 21 machi 2023, tumeorodhesha watu 310 waliuwawa wakiwemo watoto 60. Nadhani katika lugha zetu za Afrika, hatuwezi kupata maneno ya kutumia ili kutoa maana ya hali hiyo. Ituri, Kongo ni ikulu yenu ya dhahabu. Licha ya matatizo na changamoto, tuungane. Damu ni nyingi, mateso ni mengi, hali hiyo inatakiwa kusimama”, alibaini.
Baadhi ya mashirika ya kutetea haki za watoto yanaomba ulinzi kwa watoto upewe kipau mbele na viongozi na pia makundi ya silaha.
You might also like
Musenyi: Wagonjwa wa mara kwa mara walazimishwa kunusurika kwenye mabanda yenye Watu wengi
SOS Médias Burundi Musenyi, Aprili 28, 2026 — Katika kambi ya wakimbizi ya Kongo iliyoko Musenyi, wilaya ya Musongati, mkoa wa Burunga, kusini mwa taifa hilo dogo la Afrika Mashariki,
Goma: kijana mdogo uuwawa na askali polisi katika kituo cha kuandika wapiga kura
Dieudonné Bagenda, miaka 20 aliuwawa kwa kupigwa risasi. Risasi lilimpata kichwani akiwa katika kituo cha kuorodhesha wapiga kura cha Byahi alhamisi hii katika kata ya Bujovu ndani ya mji wa
Bijombo: Kijana wa jamii ya Banyamulenge afariki dunia baada ya kupigwa na jeshi la Burundi
SOS Médias Burundi Bukavu, Agosti 26, 2025 – Mutabazi, kijana wa miaka ishirini kutoka jamii ya Banyamulenge, alifariki Jumatatu, Agosti 25, baada ya kushindwa na mapigo yaliyosababishwa na wanajeshi wa
