Nyarugusu (Tanzania) : wakimbizi wawili kutoka Burundi wakufa kutokana na na maji ya mvua
Mvua kubwa zilizonyesha katika mkoa wa Kigoma (kaskazini magharibi mwa Tanzania) ambako kunapatikana kambi ya Nyarugusu nchini Tanzania zilisababisha vifo vya watu. Nyumba nyingi zilibomoka. Angalau wakimbizi wawili walifariki baada ya kusombwa na maji. HABARI SOS Médias Burundi
Mvua kubwa zilizosababisha madhara hayo zimedumu kwa wiki moja.
” Muhanga wa kwanza, ni mtoto wa miaka mitano. Alianguka katika mfereji na kupelekwa moja kwa moja na maji ya mvua katika zone 12. Muhanga wa pili ni mtu mzima mkaazi wa zone 13. Yeye alianguka katika mto Nyarugusu uliojaa na kufurika . Miwili wake uliokolewa katika eneo la makutanio ya mito Nyarugusu na Muyovozi karibu na kambi” alitoa ushahidi huo mkimbizi mmoja ambaye alizidi kuwa wawili hao wote walikuwa wakimbizi kutoka Burundi.
Mvua hizo pia ziliharibu mashamba na kubomoa nyumba na madarasa ya shule.
” Ma kumi na hata ma mia ya wakimbizi walisalia bila makaazi. Mbaya zaidi ni viongozi wa kambi kupiga marufuku kazi za kukarabati nyumba hizo. Tunajiuliza hatma ya waathiriwa hao “, vyanzo vyetu vinahakikisha na kusisitiza kuwa wanahitaji misaada ya dharura.
Katika kila msimu wa mvua, kambi ya Nyarugusu inakabiliwa na mafuriko kutokana na mahali ilipojengwa.
Kambi hiyo inawapa hifadhi zaidi ya wakimbizi laki moja na elfu 29 wakiwemo warundi elfu 51 wengine wanaosalia wakiwa ni kutoka Kongo.
You might also like
DRC (Kalehe) : watoto saba wafariki dunia kwa kuteketezwa na moto ulioibuka katika kambi ya wahanga wa mafuriko
Watoto saba wa angalau miaka mitano walifariki dunia katika ajali ya moto uliovamia kambi ya wakimbizi ya wahanga wa mafuriko ya mwezi mei iliyopita. Zaidi ya nyumba 400 ziliungua katika
Wavulana wanne waokolewa katika usafirishaji haramu wa binadamu kati ya Burundi na Tanzania
SOS Médias Burundi Rumonge, Oktoba 3, 2025 — Vijana wanne kutoka kusini mwa Burundi walirejeshwa makwao Jumatatu hii baada ya kuwa wahasiriwa wa mtandao wa ulanguzi wa binadamu unaofanya kazi
Tanzania: Kambi ya Nduta yaondolewa kwa nguvu, wakimbizi wa Burundi wafukuzwa huku kukiwa na ghasia na kimya
SOS Médias Burundi Kigoma, Aprili 27, 2026 — Katika kambi ya Nduta, iliyoko katika mkoa wa Kigoma kaskazini-magharibi mwa Tanzania, maelfu ya wakimbizi wa Burundi wanashutumu kufukuzwa kwa lazima chini
