DRC (Kalehe) : watoto saba wafariki dunia kwa kuteketezwa na moto ulioibuka katika kambi ya wahanga wa mafuriko
Watoto saba wa angalau miaka mitano walifariki dunia katika ajali ya moto uliovamia kambi ya wakimbizi ya wahanga wa mafuriko ya mwezi mei iliyopita. Zaidi ya nyumba 400 ziliungua katika kambi ya Mushonezo eneo la Kalehe mkoa wa kivu kusini mashariki mwa DRC. HABARI SOS Médias Burundi
Nyumba zilizoteketea zilikuwa na paa la nyasi.
” Hatukuokoa kitu. Hakuna aliyefanikiwa kuokoa chochote kile ” alibaini Mushagalusa , mkimbizi wa Kalehe.
Amani alinusurika na mafuriko ya Nyamukubi mwezi mei uliopita. Alikuwa katika kambi mpya ya Mushonezo. Alipoteza kila kitu katika nyumba yake.
Thomas Bakenga mkuu wa wilaya ua Kalehe, alitangaza kuwa wahanga wote ni watoto wa chini ya miaka mitano.
Mkuu wa wilaya ya Kalehe anahakikisha kuwa serikali imo mbioni kujenga nyumba eneo la Lwako na Mushonezo kwa ajili ya kuwapa hifadhi waathiriwa na janga la Nyamukubi na Bushushu tarehe 4 mei iliyopita.
Takwimu zinazotolewa na serikali ya Kongo zinaonyesha kuwa katika mafuriko yaliyoathiri maeneo ya Nyamukubi na Bushushu katika wilaya ya Kalehe mwezi mei , watu zaidi ya 400 waliuwawa na wengine 5000 kupotea.
You might also like
Kirundo : mvulana mmoja alifariki dunia baada ya kupigwa na Imbonerakure
Ezéchiel Ntahinduka, miaka 14 alifariki jumatatu tarehe 24 julai akiwa kwenye hospitali ya mkoa. Kwa mjibu wa mashahidi, kijana huyo wa kiume alifariki kutokana na kipigo aliyefanyiwa na Jean Marie
Burundi: Upinzani wasusia na mivutano inayozunguka mchakato wa uchaguzi kabla ya 2027
SOS Médias Burundi Bujumbura, Mei 9, 2026 — Huko Bujumbura, mji mkuu wa kiuchumi wa Burundi na nyumbani kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa na serikali kuu, mchakato wa uchaguzi
Gitega: mtu aliyekufa katika mazingira yasiyojulikana
Mwili wa Fabrice Nimpagaritse, 22, ulipatikana Jumatatu Julai 15 ukining’inia juu ya mti. Ugunduzi wa macabre ambao SOS Médias Burundi ilijifunza Alhamisi hii ulifanyika katika wilaya ya Yoba katika mji
