DRC (Mulongwe) : wakimbizi wanaotafuta kuuni za kupikia waathiriwa na ubakaji

DRC (Mulongwe) : wakimbizi wanaotafuta kuuni za kupikia waathiriwa na ubakaji

Katika kambi ya wakimbizi wa Mulongwe ndani ya mkoa wa Kivu kusini mashariki mwa jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, wakimbizi wanakabiliwa na ukosefu wa kuuni za kupikia. Wakimbizi hao hususan akinamama na wasichana wanakwenda hadi katika misitu ya karibu kutafuta kuuni. Kwa mjibu wa vyanzo kutoka viongozi katika jamii, wengi wao wanabakwa na watu wanaobebelea silaha na kunyanganywa simu zao pamoja na vifaa vya kukata kuni. HABARI SOS Médias Burundi

Kulingana na vyanzo ndani ya kambi, akinamama wakimbizi wanakwenda kutafuta kuuni ndani ya misitu ya Kaseke na Katalukulu. Ni katika misitu hiyo ambapo wanawakuta wanaume wanaobebelea silaha kama alivyofahamisha B.Marie mama wa watoto watano.

” Tunatembea kwa takriban kilometa 6 na miguu. Baadhi yetu wanabakwa ndani ya msitu huku wengine wakinyanganywa simu zao”.

Habari hizo zinathibitishwa na Deo Ntakirutimana kiongozi wa wakimbizi wenye uraia wa Burundi ndani ya kambi ya Mulongwe.

Kwa mjibu wake, kuna watu wanaoingia musituni kutafuta kuuni za kupikia lakini wanakuta matatizo hasa ubakaji.

Kutokana na ukosefu wa kuuni za kupikia, baadhi ya wakimbizi wanatumia nyasi ili kupika chakula.

Kambi ya wakimbizi ya Mulongwe inawapa hifadhi zaidi ya wakimbizi kutoka Burundi elfu 10.

Previous Cibitoke : wafungwa wawili wafariki wakiwa katika gereza la polisi ya mkoa
Next Gitega : hakuna sheria miaka 27 baada ya mauwaji ya askofu Joachim Ruhuna

You might also like

Wakimbizi

Aligeuka nyuma na kukwama mpakani: Mateso ya wakimbizi wa Kongo wanaokabili Imbonerakure na polisi.

SOS Médias Burundi Bujumbura, Septemba 9, 2025 – Tangu Jumatatu, Septemba 8, 2025, mamia ya wakimbizi wa Kongo wamekamatwa katika maeneo mbalimbali katika tarafa za Cibitoke na Bukinanyana, katika mkoa

Wakimbizi

Dzaleka (Malawi): kutoweka kwa viongozi wawili wa jumuiya ya wakimbizi

SOS Médias Burundi Dzaleka, Mei 27, 2025 – Wanachama wawili mashuhuri wa jumuiya ya wakimbizi katika kambi ya Dzaleka, Malawi, wametoweka tangu Jumapili. Hao ni Daniel, chifu wa kijiji cha

Wakimbizi

Musa: Kambi ya Wakimbizi Isiyo na maji kwa miezi sita, mgogoro wa kibinadamu wazidi kuwa mbaya

SOS Médias Burundi Kiremba, Juni 11, 2026 – Hali ya kibinadamu inazidi kuwa ya kutisha katika kambi ya wakimbizi ya Musasa, katika wilaya ya Kiremba ya jimbo la Butanyerera, kaskazini