Burundi: Mashirika yasiyokuwa ya hisani yalazimishwa kutoa nauli viongozi tawala ili kuwasili uwanjani

Burundi: Mashirika yasiyokuwa ya hisani yalazimishwa kutoa nauli viongozi tawala ili kuwasili uwanjani

Washirika wanaohudumu katika maeneo yoyote ya nchi sasa wataanza kuandaa bajeti kwa ajili ya kugharamia ziara za viongozi tawala. Hayo ni kwa ajili ya kuwawezesha kufika uwanjani kukagua hatua iliyopigwa katika kutekeleza wa miradi. Uamzi huo ulichukuliwa jumatatu hii katika mkutano kati ya waziri mkuu Gervais Ndirakobuca na magavana wa mikoa.
Wawakilishi wa mashirika yasiyokuwa ya serikali wanasema ni aina ya rushwa inayohalalishwa. HABARI SOS Medias Burundi

Katika baadhi ya mikoa, magavana tayari wameanza kuwapa taarifa wahusika. Mfano ni katika tarafa ya Rumonge kusini magharibi mwa nchi.
Gavana wa mkoa huo aliitisha mkutano na washirika hao wa kiufundi na kiuchumi wanaohudumu katika mkoa huo baada ya kikao na waziri mkuu mjini Gitega ( jiji kuu la siasa)
Consolateur Nitunga aliwambia kuwa sasa wataanza kufadhiri ziara zao wakiwasili uwanjani lakini pia na zile za wakuu wa tarafa.
Lengo la ziara hizo za viongozi ni kushuhudia miradi na hatua za utekelezwaji wa miradi ya mashirika hayo yasiyokuwa ya kihisani.
Washirika hao wa kiufundi na kiuchumi wanalazimika kutangaza rasmi kiwango cha pesa iliyotengwa kwa ajili ya kutekeleza mradi katika eneo fulani. Hayo ni kwa ajili ya kupata urahisi katika kupanga bajeti inayotakiwa ili kuwawezesha viongozi tawala kuwasili uwanjani.

Mashirika hayo yanatakiwa kuonyesha wazi miradi inayotekelezwa ndani ya kila tarafa ou mkoa.
Hatua hiyo imekosolewa na wawakilishi wa mashirika hayo yasioyokuwa ya kiserikali mkoani Rumonge. Baadhi walitangaza kuwa ni aina ya rushwa iliyohararishwa. Wanazidi kuwa baadhi ya magavana wa mikoa huwalazimisha wasimamizi wa miradi kuwapa kiwango fulani cha pesa pasina sababu yoyote. Wengine huomba kiwango kikubwa cha mafuta ya gari huku mafuta hayo mara baada ya kutolewa yanaishia kwenye soko la kienyeji la bidhaa hiyo.

Washirika hao wanahakikisha kuwa hali hiyo itasababisha madhara makubwa katika utekelezwaji wa miradi ya maendeleo hasa kwamba hakuna mfadhiri hata mmoja anayeweza kupanga bajeti kwa ajili ya kuwapa nauli viongozi wanaowasili uwanjani.

Wanadai kuwa ni jambo lisiloeleweka kufadhi mradi pamoja anayenufaika na mradi wenyewe.

Ifahamike kuwa katika mkutano huo wa waziri mkuu na wakuu wa mikoa wa tarehe 17 oktoba, sekta nne zilipewa kipau mbele.

Sekta hizo ni afya, maji safi na usanifishaji, kilimo, ufugaji na mazingira pamoja pia na elimu na utamaduni, utawala bora na haki za binadamu.

Previous Bubanza: Mbunge Fabien Banciryanino aibua mjadala
Next Tanzania : viongozi tawala wawahamasisha wakimbizi kuhusu kuheshimu sheria ambazo wao wanazikiuka kila mara