Kiliba : mwananchi ameuwawa na askali jeshi
Tukio hilo lilijiri katika eneo la Kiliba katika mkoa wa Kivu kusini mashariki mwa DRC siku ya jumanne. Aliyehusika na mauwaji hayo ni mwanajeshi wa Kongo anayehudumu katika sekta ya pili ya operesheni. Ni raia wa kawaida wa pili kuuwawa na askali jeshi katika mkoa wa Kivu Kusini kwa kipindi cha siku tano. HABARI SOS Médias Burundi
Muhusika na mauwaji pamoja na muhanga wote walikuwa walisafiri na pikipiki moja, kulingana na dereva wa pikipiki aliyekuwa akiwapeleka.
Walikuwa safarini kuelekea Sange (daima Kivu kusini).
” Mwanajeshi huyo alinilazimisha kusimama mahala fulani. Alichukuwa mfuko ambao mteja huyo mwingine alikuwa akibeba kabla ya kumpiga risasi bila kusema chochote”, alisema akiwa na huzuni.
Kwa mjibu wa muakilishi wa vijana katika eneo hilo, ” mwanajeshi huyo aligundua kuwa mwanaume waliokuwa wakisafiri pamoja alikuwa na kitita kikubwa cha pesa na alifanya kama anataka kujisaidia ili kusimamisha mwendesha pikipiki hiyo na badaye kumuuwa mashirika wake safarini”.
Msemaji wa FARDC (jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) eneo la Uvira, luteni Marc Elongo alisema kuwa hakuwa na taarifa za kutosha kuhusu tukio hilo.
” Nimesafiri kuelekea eneo la Bijombo (Kivu kusini), sina taarifa za kutosha kuhusiana na tukio hilo”, alijibu.
Ijumaa iliyopita, mwananchi mwingine aliuwawa na mwanajeshi katika mji wa Uvira. Aliyehusika na mauwaji hayo anazuiliwa katika gereza la idara ya ujasusi ya jeshi katika mji huo.
Katika kijiji cha Minembwe daima kusini mwa Kivu mtu mwingine aliuwawa na watu waliofananishwa na wajumbe wa FARDC jumatatu hii.
Mkoa wa kivi kusini umekuwa ukishuhudia mashambulizi ya watu wenye silaha na wizi wa mifugo licha ya uwepo wa muungano wa majeshi ya Kongo na Burundi waliotokomeza makundi ya silaha ya ndani na nje ya nchi tangu septemba iliyopita .
Makundi ya silaha yaliyopiga kambi katika eneo hilo la Kongo likiwemo kundi la Mai Mai yalihakikisha katika awamu ya mwisho ya mazungumzo ya Nairobi (mji mkuu wa Kenya ) kwamba ” hatuwezi kuweka silaha chini wakati makundi ya nje ya nchi hayajafukuzwa nje ya nchi yetu”.
You might also like
Kayogoro: a woman in detention for infanticide
Gloriose Ntirampeba, 35, was arrested this Tuesday, September 3 at her home on Mugeni hill in the commune of Kayogoro in Makamba province in southern Burundi. According to a police
Bujumbura : worrying strengthening of security at RTNB
Employees of the Burundi National Radio and Television (RTNB), a state-run medium, were surprised to see, this Friday morning, an important security device such as the presence of police dogs
Goma: more than 17,000 new people displaced following war between the regular army and M23 rebels
More than 17,000 displaced people have been registered in a newly created camp in the city of Goma in the province of North Kivu (eastern Democratic Republic of Congo). According
