Burundi: wakili Tony Germain Nkina aachiliwa huru

Burundi: wakili Tony Germain Nkina aachiliwa huru

Kitendo cha kumuachilia huru kilifanyika jumanne hii. Wiki moja iliyopita, mwanaharakati huyo wa Burundi alipatikana bila hatia na mahakama ya rufaa ya Ngozi (kaskazini mwa Burundi) kabla ya uamzi huo kupingwa na mahakama kuu ya Ngozi. Carina Terksakian wa IDHB anasema kuwa ” ni habari nzuri”. HABARI SOS Médias Burundi

Wakili Tony Germain Nkina alitoka jela jumanne asubuhi, vyanzo katika idara ya magereza vilihakikishia SOS Médias Burundi.

Vyanzo karibu na familia yake vilithibitisha pia kuwa aliachiliwa huru.

” Yuko huru na tayari amejiunga na familia yake” vyanzo vya karibu na familia yake vimefahamisha wandishi wetu wa kaskazini-mashariki mwa Burundi.

Kulingana na Carina Terksakian wa IDHB ( shirika la kutetea haki za binadamu nchini Burundi), ni habari nzuri.

” Ninaridhika kusikia kuwa wakili Tony Germain Nkina hatimaye aliachiliwa huru baada ya uamzi wa kumuachilia huru kuchukuliwa wiki moja iliyopita. Ni habari nzuri. Hangetakiwa kukamatwa na kufanya miaka miwili jela, lakini hatimae sheria imefanya kazi.

Katika uamzi wa kumuachilia huru, majaji mkoani Ngozi walionyesha uhuru wao sababu hakuna ushahidi wa mashtaka dhidi yake tukiachana na hukumu aliyopewa. Ni hatua muhimu kusonga mbele kuelekea sheria nchini Burundi” alisema.

Tarehe 20 mwezi disemba, mahakama ya rufaa ya Ngozi alimukuta pasina hatia pamoja na mtuhumiwa mwenzake Appolinaire Hitimana kabla ya mahakama kuu ya Ngozi kupinga uamzi huo siku moja badaye na kupendeleza hukumu ya jaji wa kwanza aliyemukatia kifungo cha miaka mitano jela na faini ya franka za Burundi milioni moja iendelezwe, hukumu ambayo ilitupiliwa mbali na mashirika mengi ya kutetea haki za binadamu na kutaja uamzi huo kama kinyume cha sheria.

Previous Bujumbura: a policeman shot a man
Next Kiliba : mwananchi ameuwawa na askali jeshi