Cibitoke : Zaidi ya wafungwa 180 ndani ya gereza ndogo ya polisi
Watu 178 wanazuiliwa ndani ya gereza ya kamishna ya polisi mkoani Cibitoke (kaskazini magharibi mwa Burundi) ambayo ina urefu wa mita 8 kwa upana wa mita 4. Idadi kubwa ya mahabusu hao wanafuatiliwa kwa makosa madogo madogo kama wizi ndani ya mashamba na makaazi. Watetezi wa haki za binadamu wanalaani mazingira hayo ya kifungo. HABARI SOS Médias Burundi
Gereza hiyo ambayo ilijengwa na CICR (shirika la kimataifa la msalaba mwekundu) , ina uwezo wa kuwapokea wafungwa 25 peke. Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali, watu wanaozuiliwa katika gereza hilo wako katika mazingira mabaya.
” Wanakosa vyoo na choo kimoja kinatumuwa na umati huo wote”, chanzo cha polisi kinafahamisha.
Wafungwa wanapeana zamu ili waweze kulala. Baadhi wanalala wakiwa wamesimama na chini kwenye ardhi. Athari ni nyingi ikiwa ni pamoja na maradhi ya utapia mlo kwa idadi kubwa ya wafungwa ambao wanasumbuka kupata chakula kutokana na msongamano wao.
Kama alivyoweza kushuhudia mwandishi wetu eneo hilo, msongamano wa wafungwa unatokana na sababu nyingi.
Gereza hiyo ni moja inayomilikiwa na mkoa huo na kuwapokea wafungwa wote kutoka tarafa sita za mkoa huo wa Cibitoke.
Chanzo katika polisi ki naitaja hali hiyo kuwa ni ngumu. Chanzo hicho kinafahamisha kuwa idadi kubwa ya watu wanaoepuka hali ya wananchi kujichukulia sheria wanaletwa ndani ya gereza hilo bila kuheshimu utaratibu kisheria.
Sababu nyingine ya msongamano huo kulingana na jaji alikuwa eneo hilo, ni kuchelewa kwa utaratibu wa kisheria na kufanya muda mwingi.
Mwanasheria huyo anatoa mfano wa baadhi ya wafungwa waliohukumiwa ambao wamemaliza kati ya miezi mitatu na sita wakati ambapo wangetakiwa kupelekwa katika gereza kuu ya Mpimba ( mji wa kibiashara) .
Hali hiyo inawakasirikisha watetezi wa haki za binadamu. Mmoja wao alisema wazi kuwa ” mazingira ya gerezani yanatakiwa kuheshimu viwango vya heshma kwa binadamu”.
Anaomba wizara ya sheria kutafuta suluhu ya tatizo hilo ambalo limedumu na hivyo kukiuka haki za wafungwa.
Mwendeshamashtaka katika korti kuu ya mkoa wa Cibitoke anafahamisha kuwa ” ukosefu wa gari kwa ajili ya kuwapeleka wafungwa mjini Bujumbura ndio sababu ya msongamano ndani ya gereza”.
Anaomba mashirika ya kihisani ambayo yanahudumu katika sekta ya haki za binadamu na wadau wengine ” kuwasaidia kwa kuhakikisha usafiri wa wafungwa hao”.
Kulingana na kauli yake, ni kawaida kuchukuwa hatua za kuwaachilia huru wafungwa ili kupunguza msimamo lakini hali hiyo haibadiliki.
Akihojiwa kuhusiana na hali hiyo, gavana wa mkoa wa Cibitoke, alifahamisha kuwa anataraji kuongoza mkutano kati ya viongozi wa sekta ya sheria na polisi ili kujaribu kuchukuwa hatua kukabiliana na changamoto hiyo.
You might also like
Goma: mahakama ya kijeshi yaahirisha kesi ya kigogo wa Lucha
Kesi dhidi ya Mwamisyo Ndungo mwanaharakati ya vuguvugu la LUCHA ndani ya mkoa wa Kivu kaskazini iliotaraji kusikilizwa jumatano saa nne, iliahirishwa katika siku nyingine, korti ya kijeshi mkoani humo
Burundi: ACG CIRIMOSO inashutumu kukamatwa kwa manusura wa Kitutsi walioalikwa kwenye mkutano wa kumbukumbu jijini Nairobi
SOS Médias Burundi Bujumbura, Juni 16, 2025 – Wawakilishi watatu wa vyama vya manusura wa mauaji ya kimbari nchini Burundi walikamatwa Ijumaa iliyopita walipokuwa wakijiandaa kusafiri hadi Kenya kuhudhuria mkutano
Burundi: Zaidi ya wahasiriwa 180 wa ukiukaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji zaidi ya 110 katika miezi mitatu, kulingana na Ligi ya Iteka.
SOS Médias Burundi Bujumbura, Aprili 19, 2026 — Umoja wa Haki za Kibinadamu wa Iteka umetoa ripoti ya kutisha kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Burundi katika robo ya
