Cibitoke : watu watano wenye asili ya Rwanda wanaobebelea silaha waliuwawa katika mapigano na jeshi la Burundi ndani ya msitu wa Kibira
Milio ya silaha nzito ilisikika tangu ijumaa iliyopita ndani ya msitu wa hifadhi wa Kibira kwenye milima ya Gasenyi na Gafumbegeti tarafani Mabayi mkoa wa Cibitoke (kaskazini-magharibi mwa Burundi). Kwa mujibu wa wanajeshi wanaofanyia kazi katika msitu huo, waasi watano wa Rwanda waliuwawa. Wakaazi wa maeneo ya karibu wanasema kuwa wamejawa na hofu. Wanaomba usalama uweze kuimarishwa. Mwanajeshi wa cheo, anayehusika na operesheni za jeshi katika tarafa za Mabayi na Bukinanyana anawatuliza wananchi hao. HABARI SOS Médias Burundi
Kulingana na vyanzo katika taasisi za usalama, wakati wa doria ndani ya msitu wa Kibira, wanajeshi walifungua moto na kuwapiga risasi kundi la watu wenye silaha wanaochimba madini kinyume cha sheria ndani ya msitu huo. Watano kati yao waliuwawa na wanne walijeruhiwa vikali.
Miili ya waliofariki ilitambuliwa. Ni wajumbe wa kundi la silaha wanaozungumza Kinyarwanda ambao wamepiga kambi eneo hilo kwa kipindi cha makumi ya miaka.
Walizikwa ndani ya msitu huo siku ya jumatatu. Majeruhi wanapata matibabu ndani ya hospitali moja ya mjini Bujumbura, mji mkuu wa kibiashara.
Kati kati ya mchana, siku hiyo ya jumatatu, muili wa mwanajeshi mmoja wa Burundi uligunduliwa eneo hilo pamoja na wanajeshi wengine wawili waliojeruhiwa vikali. Walipelekwa mjini Bujumbura.
Taarifa kutoka maeneo hayo zinasema kuwa kuna kundi la watu wenye silaha lililojipa kazi ya uchimbaji madini na biashara ya mbao kutoka miti ya msitu huo.
Milio hiyo ya risasi ilisababisha hofu kubwa kati ya wananchi wakaazi wa maeneo ya karibu na msitu huo.
Hii ni baada ya kundi la silaha kutoka Rwanda la FLN kuripotiwa ndani ya msitu huo baada ya zaidi ya miezi miwili ya utulivu. Vyanzo eneo hilo vinaarifu kuwa kundi hilo linajiandaa kutekeleza shambulio dhidi ya Rwanda.
Afisa wa jeshi wa cheo anayehusika na operesheni za jeshi anawatuliza wananchi. Anawahakikishia usalama wananchi wakaazi wa tarafa za Mabayi na Bukinanyana.
Hata hivyo, anatahadharisha kuwa hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia ndani ya msitu kwa ajili ya kufanya shughuli yoyote. Kuna hatari ya kumufananisha na watu wanaobebelea silaha.
You might also like
Burundi: kwanini viongozi wa Burundi wanataka kuweka taarifa za wanajeshi waliopewa dhamana ya DRC?
Waziri wa Burundi anayehusika na ulinzi Alain Tribert Mutabazi alikataa Ijumaa iliyopita kutoa maelezo kuhusu ujumbe wa FDNB (Jeshi la Ulinzi la Kitaifa la Burundi) katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Mahama: Kiboko muuaji ashambulia tena, wakimbizi wawili wa Burundi wafariki
SOS Médias Burundi Mahama (Rwanda), Mei 15, 2025 – Wakimbizi wawili wa Burundi, mwanamume wa miaka sitini na mwanafunzi wa miaka 22, hivi karibuni walipoteza maisha katika mashambulizi tofauti ya
Mpanda: maiti iliyokutwa kwenye shamba la michikichi
Mwili wa Emmanuel Hakizimana ulipatikana katika shamba la michikichi lililopo eneo la Musenyi. Iko katika wilaya ya Mpanda katika jimbo la Bubanza (magharibi mwa Burundi). Mshukiwa amekamatwa. HABARI SOS Media
