Uganda : Ngoma za asili za Burundi zinaelekea kupigwa marufuku nchini Uganda

Uganda : Ngoma za asili za Burundi zinaelekea kupigwa marufuku nchini Uganda

Ubalozi wa Burundi mjini Kampala Uganda umetoa tamko la kukataza kucheza ngoma kwenye ardhi ya Uganda. Ubalozi huo umewaamuru ma kundi ya wachezaji wa ngoma za asili nchini humo kurudisha ngoma zao kwenye ubalozi. Ofisi hiyo inalaani mwenendo ambao inasema haufai ulionyeshwa na wapiga ngoma hizo.Hata hivyo wachezaji hao ambao wengi wao ni wakimbizi hawakubaliani na hatua hiyo.

HABARI YA SOS Médias Burundi

Tamko la ubalozi wa Burundi nchini Uganda liko wazi.

“Kutokana na kosa la wapiga ngoma za asili wa Burundi nchini Uganda, tunachukuwa hatua ya kusimamisha kwa muda shughuzi zote za wacheza ngoma za asili nchini Uganda hadi watakapofanya mfumo mpya unaoheshimu sheria za desturi za ngoma za asili ambazo zimeorodheshwa kama hifadhi muhimu ya kiimila na shirika la Unesco”, ameandika Epiphanie Kabushemeye Ntamwana balozi wa Burundi nchini Uganda.

Imekuwa fursa kwa balozi wa Burundi kuwaalika katika mkutano makundi yote ya wapiga ngoma wanaoishi nchini Uganda.

“Mkutano wa makundi ya wapiga ngoma wa Burundi unapangwa kufanyika alhamisi tarehe 6 octoba 2022 kwenye ofisi ya ubalozi wa Burundi mjini Kampala kuanzia saa nne za asubuhi. Mnatakiwa kuleta ngoma ili zihifadhiwe kabla ya kutolewa muongozo wa matumizi sahihi ya ngoma hizo” linazidi tamko la ubalozi.

Kulingana na walengwa , ubalozi umejidanganya.”Natumai kuwa balozi hajamanisha sisi”. Anahakikisha kiongozi wa kamati ya wakimbizi mjini Kampala. “Hatuna uhusiano wowote na ubalozi wa nchi tangu tulipokimbia nchi ya Burundi. Siwezi kuingia ubalozini tukiacha kuhudhuria mkutano, hiyo ni kama vile nitakuwa nimerudi nchini wakati ambapo sio muda wa kurejea nchini burundi” alibaini Damien Nyabenda .

Ama kuhusu ombi la kupeleka ngoma kwenye ubalozi, wakimbizi wanapinga.

” kwanza kabisa ubalozi ungetupongeza kwa sababu makundi ya wacheza ngoma yanawazuia vijana kuzurura na kutumia madawa ya kulevya.Harafu kurudisha ngoma zetu ni jambo lisiloeleweka na pia haliwezekani. Hawakuchangia lolote katika kununua ngoma hizo. Kamwe hatutaingiza mguu wetu kwenye ofisi ya ubalozi” anaunga mkono msimano huo Bwana Mamert muanzilishi wa moja kati ya makundi ya wacheza ngoma mjini Kampala ambaye anazidi kuwa hawakualikwa rasmi kwenye mkutano.

Mtazamo ni kama huo huo katika kampi ya Nakivale

” Hapa Nakivale pia tuko na makundi wa wacheza ngoma wanaosaidia kukumbuka nchini yetu na mila zetu. Tunatupilia mbali tamko hilo la ubalozi wa nchi yetu iliyotukimbiza. Hatujuwani kwa hiyo hatuwezi kuelewana ” mmoja kati wa wapiga ngoma wa Burundi anasema.

kamati ya wakimbizi mjini Kampala yenyewe inakwenda mbali.

“Kunizua kucheza ngoma ni kama kunizua kuongea Kirundi( lugha rasmi ya Burundi) lugha mama. Hakuna kuwasiliana kuhusu mfumo wa kuenzi mila na ubalozi wa nchi iliyoninyanyasa ” Hakusita kukumbusha Damien Nyabenda.

Chanzo cha mgogoro……

Malalamiko ya Burundi yanatokana ” Nyege-Nyege festival” tamasha lililofanyika kuanzia tarahe 15 hadi 18 mwezi uliopita wa septemba katika kanda ya Jinja kusini mwa Uganda.

kundi moja la wapiga ngoma za asili wanaoishi nchini Uganda lakini wakimbizi walishiriki katika tamasha hilo.

Picha na video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha mwanamke akipiga ngoma na matiti yake yaliokuwa nje akivaa sketi fupi ou nguo zinazoonyesha sehemu nyeti za muili wake kama matiti, kitovu na makalio yake”

Mwenendo huo haukufurahisha Burundi.

Wizara ambayo katika majukumu yake inahusu vijana na mila ililaani ” Uzembe wa wacheza ngoma wa Burundi waliomuruhusu mwanamke huyo kupiga na kucheza ngoma za asili wakikumbuka kuwa ni marufuku kulingana na mila na desturi .”

” Ni aibu kwa taifa la Burundi wakati ambapo ngoma za Burundi ziliorodheshwa kama hifadhi ya kitamaduni inayolindwa na UNESCO ” wizara ya Burundi inayojihusika na utamaduni ililaani.

Pamoja na hayo mwenendo huo ulilaaniwa pia na makundi ya wakimbizi wacheza ngoma nchini Uganda.

” Tunawaomba wacheza ngoma wote kuheshimu mila na desturi za ngoma. Pia ambaye atakiuka tamaduni za ngoma aadhibiwe na kuchukuliwa hatua binafsi” wanathibitisha .

Ngoma za Burundi ziliorodheshwa kama hifadhi ya kitamaduni kwenye shirika la Unesco tangu novemba 2014.

kucheza ngoma ni sherehe inayochanganya mgurumo wa ngoma michezo na nyimbo za kitamaduni. Wananchi wote wa nje na ndani wanakubaliana kuwa ngoma ni moja kati ya nguzo ya utamaduni na utambulisho wao.

Previous Bujumbura : A senior army officer missing
Next Burundi : gorillas sold or slaughtered in the Kibira natural reserve