Burundi : Chama cha CNL kimezuiliwa kuandaa siku maluum ya vijana

Burundi : Chama cha CNL kimezuiliwa kuandaa siku maluum ya vijana

Chama kikuu cha upinzani cha CNL kilipanga kuandaa ijumapili hii siku ya kimataifa ya vijana wake. Wizara inayohusika na mambo ya ndani ilitupilia mbali ombi hilo na kudai kuwa siku maluum ya vijana wote tayari ilifanyika mwaka huu. Agathon Rwasa kiongozi wa chama cha CNL anasema hatua hii ni ya “udikteka uliozidi “. HABARI ya SOS Medias Burundi

Kulingana na barua ya katibu anayehusika mambo ya ndani na maendeleo ya ummaa, siku ya kimataifa ya vijana ya wafuasi wa chama cha CNL haingeweza kufanyika. Sababu ni moja : Siku ya kimataifa ya vijana iliadhimishwa tayari mkoani Ngozi kaskazini, sherehe zilifanyika tarehe 12 mwezi uliopita wa agosti.

Calinie Mbarushimana aliwasihi viongozi wa chama hicho cha upinzani nchini Burundi kuwahamasisha vijana wao kuitikia kwa wengi sherehe za siku kama hiyo mwaka ujao.

Agathon Rwasa kiongozi wa chama anasema kuwa hatua hiyo ni “ubaguzi mtupu”. anaona kuwa ni ” udikteka uliozidi”

“Ninaona kuwa ni njia nyingine ya kuonyesha udikteta unaozidi kuimarika katika nchi hii. Hoja zilizotolewa na viongozi wanaohusika haina msimamo. Ni maskitiko kuona wanafanya namna hiyo” analalamika bwana Rwasa.

na kuendelea “[….], chama cha CNDD-FDD ni chama kama vyama vingine, tunawaona wakifanya mandamano hapa na pale, kuhusu haya na yale. Kama una utawala, unaweza kuutumia gisi unavyotaka lakini ni muhimu kuzingatia kuwa kwa wakati mmoja madaraka yanaisha. Hakuna utawala wa milele, bora kuhudumia jamii iwapo uko kwenye utawala”.

Nchini Burundi, vyama vya kisiasa vyote vina matawi ya vijana wafuasi wao. CNDD-FDD na CNL vyote vilivyokuwa makundi ya waasi wa Hutu wako na matawi hayo kwa sehemu kubwa yakijumulisha waliokuwa wapiganaji wa zamani.Wamekuwa wakikabiliana mara kwa mara.Mwezi mei iliyopita, makabiliano kati yao eneo la Ruyumpu tarafani kiremba ( tarafa ya asili ya Agathon Rwasa) katika mkoa wa Ngozi kaskazini mwa Burundi, yalisababisha majeruhi kadhaa kwa pande zote mbili.

Takriban wapinzani saba wanatumikia kifungo cha miaka 15 katika gereza la mkoa. Walipatikana na kosa la ” jaribio la kufanya mauwaji”.

Previous DRC (Beni) : Shambulio jingine la waasi wa ADF limewauwa makumi ya watu eneo la Banande-Kainama
Next Makamba: Vijana Imbonerakure wahamishwa nje ya shule ya Makamba