Kivu-Kaskazini: mashirika ya kujitolea ya ndani yanatahadharisha juu ya mazingira mabaya ya maisha ya waliokimbia vita ya Rutshuru

Kivu-Kaskazini: mashirika ya kujitolea ya ndani yanatahadharisha juu ya mazingira mabaya ya maisha ya waliokimbia vita ya Rutshuru

Shirika la shughuli za kijamii kwa ajili ya maendeleo ya wote ASDI- RDC hivi karibuni lilifanya ziara kwenye kituo cha wakimbizi wa ndani eneo la Rwasa 2 katika wilaya ya Rutshuru. Ni katika mkoa wa kivu kaskazini mashariki mwa DRC. Katika ziara hiyo shirika hilo linafahamisha kuwa lilishuhudia kuwa wakimbizi hao wanaishi katika mazingira mabaya tangu vita kati ya jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo na waasi wa kundi la M23 kuanza. HABARI SOS Médias Burundi

Viongozi wa shirika hilo la ASDI-RDC wanathibitisha kuwa wakimbizi hao hawana chochote.

” Dharura kwa waathiriwa hao ni kuwapa msaada wa chakula, matibabu, elimu na wa kiusalama” walisema hayo.

Kituo cha Rwasa 2 kinawapa hifadhi takriban familia elfu saba. Ni wakimbizi wa vita na wakimbizi raia wa Kongo waliofurushwa kutoka Uganda.

” Tuko kwenye hatua ya kukadiria mahitaji ya wakimbizi hao wa ndani. Ni zoezi la msingi linalotuwezesha kujuwa aina ya mahitaji muhimu ya watu hao. Kwa wakati baada ya kujuwa mahitaji yao na misaada iliyotolewa na mashirika mengine ya kihisani, sasa tunatathimini njia yetu ya kuwahudumia”, alifahamisha kiongozi wa shirika hilo na kuwaombea msaada kwa serikali, mashirika mengine ya kihisani na kila mtu mwenye nia ya kuwasaidia wakimbizi wa vita.

Tangu miezi mitatu iliyopita, hali ya usalama na kiutu imesalia kuwa ya kusikitisha katika maeneo mengi ya Bwisha wilaya ya Rutshuru, kivu ya kaskazini.

Kwa mjibu wa vyanzo vyetu, ma elfu ya wakimbizi wa ndani waliotoroka mapigano kati ya jeshi la FARDC na waasi wa kundi la M23 katika wilaya ya Rutshuru, wanaishi katika mazingira mabaya ndani ya vituo vya wakimbizi na familia zilizowapokea.

Kundi la M23 linadhibiti mji wa mpakani wa Bunagana tangu miezi mitatu iliyopita. Mapigano makali yaliyoibuka wiki moja iliyopita yalipelekea ma elfu ya wakaazi wengine kutoroka makaazi yao. Baadhi walielekea nchini Uganda na tayari walitumwa katika kambi ya Nakivale, mbali na mpaka.

Previous North-Kivu: a local NGO warns of poor living conditions of Rutshuru's war displaced persons
Next Rwanda-DRC: relations continue to deteriorate between the two countries of the Great Lakes of Africa