Burundi: mwanamke wa kwanza kushikilia nyadhifa ya mpatanishi

Burundi: mwanamke wa kwanza kushikilia nyadhifa ya mpatanishi

Ni Aimé Laurentine Kanyana. Waziri huyo wa zamani wa sheria ameidhinishwa alhamisi hii na wawakilishi wa mabaraza mawili ya bunge nchini Burundi. HABARI SOS Médias Burundi

Aimée Laurentine Kanyana alikuwa kwenye ushindani na wanaume watatu. Ameidhinishwa kwa kura 109 za jumla ya wabunge 120 waliohudhuria kikao. baraza la seneti limemuidhinisha kwa kauli moja.

Kanyana sasa amekuwa mwanamke wa kwanza kushikilia nafasi hiyo na kuwa mpatanishi wa tatu wa burundi.

Mashirika ya akinama yaliyozungumza na SOS Médias Burundi yakiwemo yale ya waliotoroka nchi wamemtakia mafanikio. Kadhalika mpatanishi anayemaliza muhula wake Édouard Nduwimana amemtakia mafanikio kupitia ukurasa wa Twitter.

Wakaazi wa mkoa wa Cibitoke kaskazini-magharibi mwa Burundi wana matumaini kuwa mpatanishi mpya atawasikiliza.

” Taasisi ya mpatanishi haikutusaidia chochote. Kwa mfano tulipoteza wazazi wetu katika mzozo wa 1965 hadi sasa hatujatendewa haki. Hatujarudishiwa mali zetu. Tukienda kudai haki yetu, wanatuchukulia kama wahalifu”, alilalamika mkaazi mmoja wa Rugombo.
Kwa mjibu wa mkaazi huyo wa tarafa ya Cibitoke, ” magereza yanajaa watu wasiokuwa na hatia, taasisi ya mpatanishi haifanyi kazi yake vizuri”.

Kwenye jiji kuu la kisiasa la Gitega, akinamama wengi wameridhika.

” mwanamke kawaida yake ni mpatanishi. Tuna matumaini kuwa atatekeleza jukumu lake kikamilifu ” amehakikisha mwanamke aliyekuwa karibu na jumba la baraza la seneti la Burundi.

” Matumaini yetu ni kwamba ataanzisha mazungumzo kati ya watu. Lakini pia tunataka muwakilishi wetu katika sekta ya urithi wa mwanamke ” walipendekeza akinamama walioulizwa katika barabara za mji wa Gitega.

Taasisi ya mpatanishi ni moja kati ya taasisi zilizoanzishwa kulingana na makubaliano ya Arusha ya mwaka 2000 ambayo yalimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya muongo mmoja. Mpatanishi anachaguliwa kwa muhula wa miaka sita pasina kujiongeza.

Previous Cibitoke: the police station cell holds 110 defendants in a space intended for 20 people
Next Burundi: Prime Minister suspends fishermen associations' fundraising