Kakuma (Kenya): miezi mitano pasina kupewa chakula
Wakimbizi ndani ya kambi ya Kakuma nchini Kenya wanasikitishwa na hali ya kuchelewa kwa msaada wao wa pesa kwa kipindi cha miezi mitano. Wanahakikisha kuwa ” njaa inatupiga vibaya”. HABARI SOS Médias Burundi
Wakimbizi wa kambi ya Kakuma walikwenda kutupa kadi zao za benki mbele ya ofisi za HCR kama kuonyesha hasira yao kutokana na kuchelewa kwa msaada wao.
” Jiulizeni, tunaingia mwezi wa sita. Kawaida wanatupatia shilingi 100 kila mtu na kila mwezi kwa watu wa jinsia ya kiume pamoja na shilingi 350 kwa kila mwanamke na msichana. Pesa hiyo hutusaidia kununua kuni za kupikia, chumvi, sababu au vileso kwa ajili ya usafi wa mwanamke. Kwa hiyo, wanafikiri tunaishi kivipi miezi sita pasina kupewa msaada ? ” anajiuliza raia wa Burundi eneo hilo.
Ndani ya kambi hiyo, mwanamke anachukuliwa kama chanzo muhimu cha mapato.
” Kwa sasa, wanazaa watoto wengi na kadiri unapopata watoto wengi wa kike unakuwa na bahati kubwa sababu wanapewa pesa za ziada “, wa baba katika familia wanasema kwa mizaha.
Wakimbizi waliozungumza na SOS Médias Burundi wanaomba HCR ” kutukumbuka na kutuhakikishia ulinzi” kinyume na hayo shirika hilo la umoja wa mataifa litakuwa limefeli katika jukumu lake.
HCR pamoja na mashirika mengine ya misaada katika eneo la Afrika mashariki walisema ni kutokana na tatizo la ukosefu wa ufadhili mnamo siku hizi.
Kambi ya Kakuna inawapa hifadhi zaidi ya wakimbizi laki mbili kutoka mataifa mbali mbali wakiwemo warundi zaidi ya elfu ishirini.
You might also like
Burundi: more than 70,000 Burundian refugees to be repatriated in 2023
The challenge was announced by the inspector general of the ministry for internal affairs and security on Tuesday during a visit in Nyarugusu camp. It’s under the same ministry that
Nakivale (Uganda): election of new refugee representatives
From December 14 to 16, an election was held to choose new bodies representing the refugee community at Nakivale camp in Uganda. The president is a Congolese re-elected to this
DRC : a truce announced between Kinshasa and the M23 under Qatari mediation, but fighting continues in the east
SOS Médias Burundi Despite a joint declaration announcing a truce between the Congolese government and the M23 under the auspices of Qatar, armed clashes continue in the eastern Democratic Republic
