Bijombo: wapiganaji wa kundi la Twirwaneho wamewauwa wanajeshi watatu wa FARDC

Bijombo: wapiganaji wa kundi la Twirwaneho wamewauwa wanajeshi watatu wa FARDC

Wanajeshi hao watatu waliuwawa katika mapigano kati ya jeshi la Kongo na kundi la silaha la Twirwaneho linaloundwa na vijana wa jamii ya Banyamulenge, jumanne hii. HABARI SOS Médias Burundi

Kwa mjibu wa vyanzo vya ndani, mapigano makali yalifanyika jumanne hii asubuhi kati ya wapiganaji wa kundi la Twirwaneho na wanajeshi wa FARDC ( jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo). Makabiliano yaliripotiwa katika kitongoji cha Bijombo ndani ya wilaya ya Uvira mkoa wa Kivu ya kusini mashariki mwa DRC.

” Mapigano makali yalifanyika hususan katika maeneo ya kanyaga na Irango. Maeneo hayo tuliwauwa wanajeshi watatu. Wawili wengine waliuwawa siku ya jumatatu” vyanzo vya karibu na kundi la Twirwaneho vinasema.

Msemaji wa jeshi la FARDC halipatikana kwenye simu ili kujieleza juu ya madai hayo.

Lakini wakaazi walituhumu wanajeshi wa FARDC kufanya uporaji katika maeneo walikopita baada ya kushindwa nguvu na wapiganaji wa jamii ya Banyamulenge.

Mapigano hayo yalifanyika baada ya jeshi la FARDC na FDNB ( jeshi la Burundi) kuwakamata watu watano wakiwemo raia wawili wa Burundi waliokuwa wakipeleka misaada ya vyakula kundi la Twirwaneho siku ya jumamosi iliyopita.

Wadadisi wanasema kuwa kanali Michel Makanika kamanda wa kundi la silaha la Twirwaneho anafahamu vizuri eneo hilo na wapiganaji wake wako kama nyoka ambao wako katika mashimu yao binafsi.

Previous Bujumbura: police killed three suspected thieves
Next Cibitoke: miili mingine imepatikana tarafani Rugombo

You might also like

Security

Gihanga : three police officers arrested in possession of fraudulent goods

Three police officers in a vehicle were arrested and goods in their possession seized by their colleagues. They only stopped the car after warning shots were fired this Sunday evening

Security

Bujumbura attack : Burundian authorities took official stock and accused Rwanda again

After Friday’s early evening grenade attack on a public transport bus parking lot in the commercial city Bujumbura, Burundian authorities reported 38 injured, including 5 seriously. A spokesperson for the

Society

Mkutano wa baba François na waathiriwa wa mashariki mwa DRC: maumivu yenu ni maumivu yangu (baba mtakatifu)

Mkuu wa kanisa katoliki alikutana jumatano hii alasiri na wawakilishi wa wahanga wa maovu yanayotendeka mashariki mwa Kongi ambako makundi mengi ya silaha ya ndani na nje yanaripotiwa. Aliwapokea pia