Bijombo: wapiganaji wa kundi la Twirwaneho wamewauwa wanajeshi watatu wa FARDC
Wanajeshi hao watatu waliuwawa katika mapigano kati ya jeshi la Kongo na kundi la silaha la Twirwaneho linaloundwa na vijana wa jamii ya Banyamulenge, jumanne hii. HABARI SOS Médias Burundi
Kwa mjibu wa vyanzo vya ndani, mapigano makali yalifanyika jumanne hii asubuhi kati ya wapiganaji wa kundi la Twirwaneho na wanajeshi wa FARDC ( jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo). Makabiliano yaliripotiwa katika kitongoji cha Bijombo ndani ya wilaya ya Uvira mkoa wa Kivu ya kusini mashariki mwa DRC.
” Mapigano makali yalifanyika hususan katika maeneo ya kanyaga na Irango. Maeneo hayo tuliwauwa wanajeshi watatu. Wawili wengine waliuwawa siku ya jumatatu” vyanzo vya karibu na kundi la Twirwaneho vinasema.
Msemaji wa jeshi la FARDC halipatikana kwenye simu ili kujieleza juu ya madai hayo.
Lakini wakaazi walituhumu wanajeshi wa FARDC kufanya uporaji katika maeneo walikopita baada ya kushindwa nguvu na wapiganaji wa jamii ya Banyamulenge.
Mapigano hayo yalifanyika baada ya jeshi la FARDC na FDNB ( jeshi la Burundi) kuwakamata watu watano wakiwemo raia wawili wa Burundi waliokuwa wakipeleka misaada ya vyakula kundi la Twirwaneho siku ya jumamosi iliyopita.
Wadadisi wanasema kuwa kanali Michel Makanika kamanda wa kundi la silaha la Twirwaneho anafahamu vizuri eneo hilo na wapiganaji wake wako kama nyoka ambao wako katika mashimu yao binafsi.
You might also like
Bubanza: demobilized soldiers concerned about the lack of law governing them
Grievances raised by demobilized soldiers during a meeting held this Monday in Bubanza (western Burundi) by the minister in charge of defense and veterans, accompanied by the minister in charge
Nyabibwe (South Kivu) : the M23 killed a colonel in charge of FARDC operations
Colonel Alexis Rugabisha was killed on Saturday, February 1, 2025. He died in the fighting between the Congolese army and M23 rebels in the locality of Nyabibwe. It is in
Photo of the week : threat of uncleanness related diseases at the main market
Fruit sellers at the Makamba market (south of the country) say they fear contracting diseases linked to unsanitary conditions, just like their customers. The garbage dump of this market next
