Gasorwe: mufuasi wa chama cha CNL atekwa nyara
Viateur Nzigo, mufuasi wa chama cha CNL (kongamano la kitaifa kwa ajili ya uhuru) alitekwa nyara kutoka nyumbani kwake tarafani Gasorwe mkoa wa Muyinga (kaskazini mwa Burundi) asubuhi ya jumatano tarehe 29 machi. Alitekwa na watu waliokuwa ndani ya gari ambalo wakaazi walisema ni gari la idara ya ujasusi. Tangu wakati huo, familia yake haina taarifa zake. HABARI SOS Médias Burundi
Kwa mjibu wa vyanzo vya SOS Médias Burundi tarafani Gasorwe, gari aina ya Toyota Hilux lilikuja nyumbani kwake. Aliitwa na watu waliokuwa katika gari hilo ambao wajumbe wa familia yake walisema ni askali polisi.
” Polisi hao walimuita wakati bado akilala. Kabla ya kutoka nje, Nzigo alifungua dirisha na kuangalia aliyemuita. Baada ya kugundua kuwa ni askali polisi alitahadharisha wafuasi wenzake wa chama cha CNL. Wanaume hao walimuvamia na kumuweka kwa nguvu ndani ya gari hilo ambalo lilikuwa halina pleti namba “, alifahamisha mjumbe mmoja wa familia yake.
Kulingana na chanzo hicho, polisi hao walimupeleka bila waranti wa kukamatwa, na walikuwa wakielekezwa na mtu aliyekuwa ndani ya gari hilo.
Wafuasi wa chama cha CNL waliotahadharishwa walisema kuwa gali hilo lilitambulika.
” Hakika lilikuwa gari la idara ya ujasusi ambalo lilimupeleka mwenzetu “, alifahamisha mfuasi wa chama cha CNL.
Gari lilielekea kwenye makao makuu ya mkoa wa Muyinga, lakini hadi usiku wa kuamkia jumatano , hakuna aliyekuwa na taarifa kuhusu maeneo anakozuiliwa, au iwapo bado yuko hai.
Familia yake pamoja na wafuasi wa chama cha CNL wanasema kuwa walimutafuta ndani ya magereza yote bila mafanikio. Wanaomba aachiliwe huru.
You might also like
Nyarugusu (Tanzania) : mashamba mengi ya mahindi kuharibiwa na uongozi wa kambi hiyo
Visa hivyo vimeripotiwa mwanzoni mwa wiki hii katika kambi ya Nyarugusu nchini Tanzania. Mkuu wa kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu aliharibu shamba la mahindi kwa ajili ya kupiga vita shughuli
DRC: the freedom of the press laws awaits its promulgation
The Minister for Communication and Media Patrick Muyaya won his bet on Tuesday before the country’s deputies. It’s a bill to ratify the ordinance law on the terms and conditions
Uvira : mwanajeshi mmoja na wananchi wawili wauwawa
Raia wawili wa kawaida, waliuwawa na watu wanaobebelea silaha. Na mwanajeshi mmoja wa Kongo pia aliuwawa. Waliouwawa walikuwa miongoni mwa kundi la vijana walinzi wa amani wanaofanya doria usiku. Mwanajeshi
