Bujumbura : waziri wa usalama yazindua warsha iliyoandaliwa na shirika la OLUCOME lakini wajumbe wasimamisha shughuli hiyo

Bujumbura : waziri wa usalama yazindua warsha iliyoandaliwa na shirika la OLUCOME lakini wajumbe wasimamisha shughuli hiyo

Alhamisi asubuhi tarehe 30 machi, OLUCOME (shirika kwa ajili kupiga vita rushwa na ubadilifu wa mali ya umma) chini ya usimamizi wa wizara ya mambo ya ndani, maendeleo ya jamii na usalama liliandaa warsha kuhusu sarafu ya Burundi kuzidi kushuka thamani thamani. Askali polisi chini ya amri za kanali mmoja walikuja na kusimamisha harakati hizo ambapo wadau katika sekta ya umma na binafsi walihusishwa. Shughuli hizo zilizokuwa zimepangwa kuanza saa tatu zilianza masaa mawili badaye. HABARI SOS Médias Burundi

Ma kumi ya wajumbe wa taasisi mbali mbali za umma , mashirika ya kiraia, baadhi ya wawakilishi wa vyombo vya habari pamoja na mtalaam wa maswala ya uchumi hawakujuwa la kufanya. Kwenye lango la kuingilia katika ukumbi wa mkutano huo eneo la Kabondo ( magharibi mwa jiji la Bujumbura) walikuwepo baadhi ya askali polisi akiwemo mwenye cheo cha kanali wa polisi aliyekuwa akitoa amri. Baadhi ya washiriki walikuwa ndani ya ukumbi, wengine nje. Baadhi ya watu walikuwa wakiingia ndani ya ukumbi ikionekana kuwa hawajuwi wanakokwenda au kile walichokuja kufanya. Mlinzi alijaribu kumutoa nje mtu aliyevalia nguo chafu anayeangalia huku na kule. Dakika moja badaye mtu huyo alirejea.

” Ni mjumbe wa idara ya ujasusi. Hivyo ndivyo wanavyofanya ili kusikiliza watu” alisema kwa sauti ya chini mshiriki.

Baada ya huyo, mwanaume mwingine alivaa vizuri aliingia ndani ya ukumbi na kuwasalimia washiriki kwa heshima. Ilikuwa vigumu kwake kujieleza ni nani.

” Ninatoka hapa….taasisi…mtu wa wizara….wa utawala…” alisita sana. Walimuambia kuwa kuna mjumbe wa wizara ya mambo ya ndani wakati wakimukaribisha kunywa chai katika mapumziko.

Hatimaye warsha ilianza saa tano. Gabriel Rufyiri ambaye alikuwa amemaliza kuzungumza na waziri husika alifahamisha kuwa wamemaliza kupata ruhsa ya wizara.

Baada ya warsha hiyo, Gabriel Rufyiri alikutana na wandishi wa habari kwa ajili ya ” kutuliza hali”. Alimushukuru waziri Martin Niteretse anayehusika na mashirika ya kiraia.

Kuhusu mkasa uliotokea, alifahamisha kuwa kuna watu wenye nia mbaya ambao waharidhishwi na harakati za shirika la OLUCOME na ambao wanawadanga viongozi “.

Wiki moja iliyopita, askali polisi walijaribu kusimamisha shughuli iliyoandaliwa na shirika la OLUCOME katika mji mkuu wa kiuchumi wa Bujumbura ambapo hata hivyo mjumbe wa wizara ya mambo ya ndani na usalama pamoja manispa ya jiji la Bujumbura walihudhuria.

” Mtawasikia watu kama Rufyiri wakiniomba kupitia vyombo vya habari kupunguza bei ya bidhaa za vyakula wakati hafanyi kazi yoyote. Wanasalia katika ofisi zao mjini Bujumbura na hawataki kutumika. Tunapowaomba kufuga angalau sungura watano na kwenda kulima hawatusikii. Anataka nimpe maziwa ya ng’ombe wangu au mavuno yangu ya viazi ulaya bila kulipia ? ” alikosoa rais Neva kama kutoa majibu kwa mwakilishi wa shirika maarufu sana la kupambana na rushwa na ubadilifu wa mali ya umma katika nchi hiyo ndogo ya Afrika mashariki ambaye siku chache kabla, alikuwa ameomba hatua inayowazui viongozi kufanya biashara ichukuliwe.

Na kusisitiza akijieleza mbele ya vijana katika jiji la kisiasa la Gitega. ” anatumia muda wake wote kusikiliza mizaha wa wazee. Fikra zao zilipitwa na wakaazi. Vijana tunatakiwa kuwapuuza watu hao. Wako katika dunia ya miaka 90. Wako na fikra zilizooza “

Previous Gasorwe: mufuasi wa chama cha CNL atekwa nyara
Next Goma : mandamano ya mashirika ya kiraia kwa ajili ya kupinga vurugu zinazofanyika katika vituo vya kuandika wapiga kura