Goma : mandamano ya mashirika ya kiraia kwa ajili ya kupinga vurugu zinazofanyika katika vituo vya kuandika wapiga kura

Goma : mandamano ya mashirika ya kiraia kwa ajili ya kupinga vurugu zinazofanyika katika vituo vya kuandika wapiga kura

Mandamano hayo yaliyoandaliwa na vuguvugu la wananchi la génération positive yalifanyika alhamisi hii. Shirika hilo linapinga rushwa, ushawishi na vurugu katika vituo vingi vya kuorodhesha wapiga kura katika mji wa Goma. HABARI SOS Médias Burundi

” Uraia haununuliwi. Hapana kulipia kadi ya wapiga kura”. ” Kadima toweni kadi nzuri za kupigia kura “. Hayo yalisomeka kwenye mabango ya wandamanaji.

Wajumbe wa shirika hilo wanasema kuwa hawaelewi kwa nini kadi ya kupiga kura inanunuliwa.

” Shirika hilo linapinga mpango wa tume huru ya uchaguzi CENI Kivu kaskazini wa kuwatenga baadhi ya wapiga kura wa mkoa huo katika mchakato wa uchaguzi “, alifahamisha mjumbe mmoja wa shirika hilo.

Shirika hilo liliomba muda wa kuandikisha wapiga kura uongezwe kwa angalau miezi mitatu na idadi ya vituo vya kuorodhesha wapiga kura iongezwe pia.

” Upendeleo na hali ya kutumia ushawishi ndani ya vituo vya kuorodhesha wapiga kura ni tabia ya kutupilia mbali”, alisisitiza David Wakilongo mjumbe wa shirika la génération positive.

Katika muendelezo wa mandamano hayo, wandamanaji walielekea kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa na kuonyesha mabango yao.

Waliomba viongozi kuwajibika ili ” kusimamisha tabia hiyo isiofaa” ya CENI.

” Tuko hapa kwa ajili ya kuomba gavana wa mkoa jemedali Constant Ndima asimamishe mwenendo huo wa CENI ndani ya Kivu kaskazini sababu imekuwa kero kwa akinamama wazee kumaliza zaidi ya masaa ma nane bila kufika kwenye kituo cha kuandika wapiga kura. Ni hatari sana”, alitetea Anne Marie Katungu.

” Tunaomba serikali kuchukuwa hatua zinazowahakikishia usalama wananchi na kutupatia kadi zetu za kupiga kura sababu ni haki yetu kama wananchi wa Kongo “, alisisitiza.

Wengine wanadai viongozi wangeongeza idadi ya wajumbe wa CENI ili kurahisisha mchakato huo na kuongeza kasi ya kazi hiyo.

Mbele ya ofisi ya mkuu wa mkoa, ujumbe wa shirika hilo la Génération positive kwa kifaransa ulipokelewa na gavana wa mkoa wa Kivu kaskazini. Gavana huyo aliwahikishia kuwa atatafuta suluhu kwa ajili ya kuendelea na zoezi la kuorodhesha wapiga kura kwa utulivu.

” Ninajuwa kama hamjaridhika na inaeleweka lakini nina ahidi kumaliza tatizo hilo ili sote kwa pamoja tupate suluhu la kudumu”, aliwahakikishia wandamanaji Constant Ndima Kongba gavana mwanajeshi wa mkoa wa Kivu kaskazini .

Wandamanaji wanasema kuwa hawakuridhishwa na majibu ya kiongozi wa mkoa.

” Sisi sio wa kwanza kutahadharisha kuhusiana na hali hiyo. Tutaanzisha visa vikubwa ili sauti ya mwananchi wa kawaida iweze kusikika”, alifahamisha Séraphin Lubungo.

Ma jemedali na vigogo wengine wanakuja kwenye vituo vya kuorodhesha wapiga kura na kundi la watu. Hatu hao huhudimiwa kabla ya wale waliofika tangu saa tisa za alfajiri na mwishowe, wanajikuta wakirejeshwa nyumba bila kuandikwa, ni hatari”, alilalamika Munyakasali Milina.

Ikimbukwe kuwa tangu mwanzoni mwa zoezi la kuandika wapiga kura katika mkoa wa Kivu kaskazini, idadi kubwa ya wajumbe wa mashirika ya kiraia waliendelea kupinga ujanja unaoshuhudiwa kwenye vituo vya kuorodhesha wapiga kura.

Katika mkoa jirani wa Kivu kusini hususan eneo la Kalehe, wapiga kura walipinga hali kama hiyo .

Previous Bujumbura : waziri wa usalama yazindua warsha iliyoandaliwa na shirika la OLUCOME lakini wajumbe wasimamisha shughuli hiyo
Next DRC : the Congolese army accuses Kigali of violating agreements